Nyumbani » 30/10/2013 Entries posted on “Oktoba 30th, 2013”

Brahimi bado yuko Damascus, Kaag kuhutubia Baraza la Usalama wiki ijayo

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu kuhusu Syria Lakhdar Brahimi yuko nchini humo ambapo leo amekuwa na mazungumzo na Rais Bashar Al Assad. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema tayari Brahimi amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Moallem na anaendelea na vikao [...]

30/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Fatiha Serour msaidizi mwakilishi wake nchini Somalia

Kusikiliza / Bi Fatiha Serour

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon ametangaza uteuzi wa Fatiha Serour raia wa Algeria kuwa msaidizi wa mwakilishi wake maalum kwa ajili ya Somalia Bwana Ban amemshukuru Peter De Clercq wa Uholanzi ambaye emitumikia nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM. Mteule huyo mpya Bi [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya elimu yamulikwa nchini Sudan kusini

Kusikiliza / Watoto darasani

Sudan Kusini , taifa changa linalokumbana na changmoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni elimu ya msingi. Nchini humo sio ajabu kukutana na watu wenye umri wa makamu ambao hawajui kusoma wala kuandika. Nini kifanyike? Na je nini kinakwamisha mchakato wa elimu nchini humo? Ungana Grace Kaneiya katika taarifa inayomulika hali ya elimu nchini humo.

30/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

M23 wajisalimisha, mji wa Bunagana sasa chini ya FARDC: MONUSCO

Kusikiliza / Waasi wa M23

Mnamo mwezi Oktoba, idadi kubwa ya wapiganaji wa kundi la waasi la M23 walijisalimisha kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka Utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO. Hapo jana tarehe 29 Oktoba, wapiganaji wengine 33 wa M23 walijisalimisha, na hivyo kupelekea idadi ya wapiganaji wa M23 walojisalimisha kwa MONUSCO kufika 80 katika [...]

30/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika hali nchini Somalia

Kusikiliza / Jan Eliasson

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao kuhusu hali nchini Somalia. Akikihutubia kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, amesema baada ya ziara yake nchini Somalia, amerudi na hisia za matumaini na kutiwa moyo, lakini pia kuna mengi ya kuhofia. Joshua Mmali na taarifa kamili TAARIFA YA JOSHUA Bwana Jan Eliasson, ameliambia [...]

30/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi za Afrika hazitoi ushirikiano wa kutathmini hali ya haki za binadamu: Kiai

Kusikiliza / Maina Kiai

Mtaalam maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kufanya mikutano ya amani na haki ya kujumuika, Maina Kiai, ametoa wito kwa nchi za Afrika zishirikiane naye na wenzie katika kufanya tathmini ya hali ya haki za binadamu katika nchi hizo. Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Kiai, amesema katika muktadha wa [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchini Tanzania mimba za utotoni hali yasalia tete: UNFPA

Kusikiliza / teenage-pregnancy

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFP leo limezindua ripoti yake na kuitaja Tanzania kama moja ya nchi ambazo zinakabiliwa na ongezeko kubwa la mimba za utotoni na hivyo kuwafanya wasichana wengi kukatiza masomo yao. Ripoti hiyo ambayo imeangazia hali ya idadi ya watu imesema kuwa kati ya mimba milioni moja [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahakama kuu nchini Maldives inavuruga shughuli ya uchaguzi : Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina Mkuu wa haki zaa binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasi wasi wake kutokana na mabadiliko ambayo yametokea kwenye shughuli ya uchaguzi chini Maldive kufuatia hatua ya mahaka kuu nchini humo ya kuingilia uchaguzi wa urais. Taarifa kamili na Jason Nyakundi (TAARIFA YA JASON)   Pillay amesema kuwa kuna wasi wasi mkubwa [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mimba za utotoni huathiri afya, elimu na haki za watoto wa kike: UM

Kusikiliza / adolescent_pregnancy_swp

Kila mwaka, watoto milioni 7.3 wa kike chini ya umri wa miaka 18 hushika na kujifungua mimba, imesema ripoti mpya kuhusu hali ya idadi ya watu mwaka 2013, ambayo imetolewa na Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu katika Umoja wa Mataifa, UNFPA.  Taarifa kamili na Assumpta Massoi: (RIPOTI YA ASSUMPTA) Ripoti hiyo imesema, milioni [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dini Uganda shawishini wajawazito waende kliniki: Dkt. Rugunda

Kusikiliza / Dr. Ruhukana Rugunda (katikati) akitembelea kituo cha afya cha Azur

Nchini Uganda harakati zinaendelea kufikia lengo namba Tano la Milenia la kupunguza vifo vya wajawazito ambapo Waziri wa Afya amewatolea wito viongozi wa kidini kuhimiza wajawazito kwenda kliniki. Inaelezwa kuwa idadi ya wajawazito wanaofarikidunia wakati wa kujifungua, ilishuka kutoka 435 hadi 310 kwa kila wajawazito laki moja mwaka 2010 lakini ripoti mpya nchini Uganda inaonyesha [...]

30/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031