Nyumbani » 29/10/2013 Entries posted on “Oktoba 29th, 2013”

Watetezi wa haki za binadamu kwenye miradi mikubwa huonekana "wapinga serikali":Mtaalamu maalum

Kusikiliza / Bi Margaret Sekaggya

Watetezi wa haki za binadamu wanaofanya kazi kwa niaba ya jamii zinazoathiriwa na miradi mikubwa ya maendeleo kila mara hunyanyaswa na hata kupachikwa majina ya wapinga serikali au wapinga maendeleo pindi wanapokuwa wanatekeleza jukumu hilo. Ni kauli ya Margaret Sekaggya alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York, baada ya kuwasilisha ripoti yake ya mwisho [...]

29/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahanga wa kimbunga Sandy huko Caribbean wasisahauliwe: UNDP

Kusikiliza / Kimbunga Sandy

Mwaka mmoja baada ya kimbunga Sandy kupiga maeneo ya Caribbean na pwani ya Mashariki ya Marekani, shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa limetaka kutosahauliwa kwa wahanga wa janga hilo hususan wale wa maeneo ya Caribbean. Heraldo Muñoz, Mkurugenzi wa UNDP ofisi ya Amerika ya Kusini katika tahariri yake iliyochapishwa kwenye mtandao amesema [...]

29/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakati umefika kuwa na bunge la dunia: Mtaalamu

Kusikiliza / Alfred de Zayas

Mtalaamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uendelezaji wa demokrasia na usawa duniani Alfred de Zayas ameunga mkono wito unaotolewa wa kuwa na bunge la dunia, chombo ambacho amesema kitakuwa ni jibu la pengo la kidemokrasia linalojitokeza. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi De Zayas amesema chombo hicho kitatoa fursa ya sauti ya umma kusikika kupitia wawakilishi [...]

29/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usalama na ulinzi wazorota CAR na DR Kongo

Kusikiliza / Wakimbizi wa kutoka CAR

Hofu kubwa imetanda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kufuatia mapigano ya vikundi vyenye silaha na kuitaka serikali ya mpito kuingilia katika kuimarisha usalama huku hali ya misaada ya kibinadamu ikiendelea kuzorota nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC. Akizungumza na waandishi wa habari mjini new York Mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya [...]

29/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwanamuziki wa Uchina, Lang Lang atangazwa kuwa Balozi Mwema wa Amani

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon na Mwanamziki Lang Lang

Umoja wa Mataifa una balozi mpya wa amani. Jina lake, ni Lang Lang, mcheza kinanda maarufu kutoka Uchina.  [Muziki] Na huo, ni mdundo uitwao Chopin Waltz, uloendana na hafla ya kumsimika balozi mwema wa amani. Aliyemtangaza, ni Katibu Mkuu, Ban Ki-moon  "Kwa furaha na fahari, namtangaza Lang Lang kama balozi mwema wa amani wa Umoja [...]

29/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Yaya Touré balozi mpya wa UNEP

Kusikiliza / Yaya Touré

Mchezaji wa kimataifa wa Côte d’Ivoire na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Touré ametangazwa rasmi kuwa balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP na kuahidi kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu barani Afrika. Touré ambaye alilazimika kusafiri hadi Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya kutangazwa kuwa balozi [...]

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mediterenia ya mashariki ni eneo la pili duniani kwa maafa kutokana na ajali za barabarani

Kusikiliza / Ripoti ya usalama barabarani yatolewa na WHO

Ripoti mpya kuhusu usalama barabarani kote duniani mwaka huu wa 2013, imetolewa leo na Shirika la Afya Duniani, WHO. Ripoti hiyo ambayo ina maelezo kutoka nchi 182, inaweka pia vigezo vya kufuatilia hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika mwongo mmoja wa usalama barabarani, kati ya mwaka 2011-2020. Grace Kaneiya  ana maelezo zaidi (Ripoti ya Grace)  

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yathibitisha mkurupuko wa ugonjwa wa Polio Syria

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo dhidi ya polio

Shirika la Afya Duniani, WHO, limethibitisha kuwepo mkurupuko wa ugonjwa wa kupooza wa polio nchiniSyria, ambao umwaathiri watoto wapatao kumi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Joseph Msami ana taarifa kamili. (Taarifa ya Joseph Msami) WHO imesema mkurupuko huo umethibitishwa kwenye eneo la Deir Al Zour mashariki mwa Syria, na umeathiri watoto chini ya umri wa [...]

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lapitisha azimio kuhusu uondoaji wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba

Kusikiliza / Wakati wa kikao, Baraza Kuu (picha ya faili

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kishindo azimio juu ya umuhimu wa kuondoa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba. Nchi 188 zimeunga mkono huku Marekani na Israeli zikipinga wakati visiwa vya Marshalls, Micronesia na Palau hazikuonyesha msimamo wowote. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Wajumbe [...]

29/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaonya kufuatia hatua ya kuwarejesha kwa lazima wale wanaokimbia ghasia nchini Nigeria.

Kusikiliza / Wanaokimbia mapigano kutoka Nigeria (picha ya faili)

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa raia wa Nigeria wanaokimbia ghasia kaskazini mashariki mwa nchi hawatarejeshwa makwao kwa lazima. Alice Kariuki na ripoti kamili.  (Ripoti ya Alice) Mapigano kati ya wanajeshi wa Nigeria na wanamgambo kwenye majimbo yaliyo kaskazini mashariki mwa nchi ya Adamawa, Borno na Yobe yamewalazimu hadi watu [...]

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Masuala ya uhamiaji kumuulikwa wakati wa mkutano wa IOM huko Nairobi

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Kamati kuhusu uhamiaji kwenye pembe ya Afrika na nchini Yemen inaandaa mkutano wake wa tatu mjini Nairobi nchini Kenya  kuanzia tarehe 3o hadi 31 mwezi huu. Mkutano huo unalenga kuboresha ushirikiano kati ya serikali  kwenye pembe ya Afrika na Yemen na washirika wa kimataifa katika mikakati ya kuboresha uhamiaji na hali za wahamiaji. Jumbe Omar [...]

29/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yaanzisha kampeni ya kuzuia maambukizi ya HIV miongoni mwa vijana

Kusikiliza / wanafunzi wanoshirikiana na serikali ya Kenya kuhusu elimu ya uzazi

Shirika la  Umoja wa Mataifa linalohusika na Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO limesema kuwa zaidi ya ailimia  50 ya vijana ambao tayari wamefikia umri wa kubalehe walioko katika nchi za Kusini na Afrika Mashariki hupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kila siku kutokana na kukosa elimu bora ya uzazi. Kutokana na hatua hiyo, UNESCO imeanzisha [...]

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yasalia kuwa mbaya: WFP

Kusikiliza / Msaada wa chakula kutoka WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasema hali ya uhakika wa chakula nchini Zimbabwe ni mbaya zaidi tangu uhaba wa chakula kukumba nchi hiyo mwaka 2009. WFP inasema uhaba wa chakula unatokana na sababu kadhaa ikiwemo hali mbaya ya hewa, gharama kubwa ya mbolea na hata upatikanaji wake ni wa taabu pamoja na kupanda [...]

29/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930