Nyumbani » 28/10/2013 Entries posted on “Oktoba 28th, 2013”

Baraza la usalama lalaani shambulio la M23 dhidi ya MONUSCO

Kusikiliza / Gerard Araud, Mwakilishi wa kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu limekuwa na kikao cha dharura na faragha kuhusu hali ilivyo Mashariki mwa DR Congo ambako mapigano mapya yamezuka Ijumaa alfajiri kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 na kusababisha vifo. Taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho imekariri wajumbe wakilaani vikali mashambulio yaliyofanywa na M23 dhidi [...]

28/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Awamu ya kwanza ya kuthibitisha silaha za kemikali nchini Syria yakamilika:

Kusikiliza / Wakaguzi wa ujumbe wa pamoja wa UM-OPCW

Ripoti kutoka The Hague, Uholanzi zinasema kuwa wataalamu katika timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali, OPCW wamehitimisha awamu ya kwanza ya kukagua na kuthibitisha silaha za kemikali nchini Syria.  Inaelezwa kuwa hadi Jumapili tarehe 27 mwezi huu, wataalamu walishakagua na kutambua maeneo 21 [...]

28/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto wa kike hawaendi shule kila mwezi kwa kukosa vifaa vya kujisafi: Mtaalamu huru

Kusikiliza / Catarina de Albuquerque

Kamati za Baraza kuu la Umoja wa Mataifa zimekuwa na vikao vyake mjini New York siku ya Jumatatu ambapo miongoni mwao ni ile ya Tatu inayohusika na undelezaji na ulinzi wa haki za binadamu iliyohusisha wataalamu maalum kuwasilisha ripoti zao za mwaka. Catarina de Albuquerque alikuwa mmoja wao ambaye ripoti yake iligusia haki ya kupata [...]

28/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Lang Lang balozi mpya wa amani wa UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Lang Lang

Mwanamuziki chipukizi kutoka China Lang Lang ameidhinishwa rasmi kuwa balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa tukio lililofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu Ban Ki-moon ambaye licha ya kumsifia mwanamuziki huyu anaainisha majukumu yake akiwa balozi wa amani.   “Lang Lang atafanya kazi nasi katika [...]

28/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yamulikwa jimbo la Abyei

Kusikiliza / Omar Al-Bashir wa Sudan na  Salva Kiir wa Sudan kusini

Wakati wajumbe wa baraza la usalama na amani la Muungano wa Afrika, AU wakikamilisha ziara yao katika jimbo la Abyei nchini Sudan jimbo ambalo limeshuhudia migogoro kwa muda mrefu. Wakati ziara hiyo ikijiri, wakuu wa mataifa mawili , Sudan na Sudan Kusini wamekutana katika mchakato wa kuhakikisha amani inarejea jimboni humo. Ungana na Joseph Msami [...]

28/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi zaidi kutoka DRC wamiminika nchini Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka DRC

  Zaidi ya watu 3,000 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamekimbilia nchi jirani ya Uganda baada ya vijiji vyao kushambuliwa na waasi wanaodaiwa kuwa ni wa M18. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, ana ripoti kamili. (Tarifa ya John Kibego)  Wakimbizi hao ambao wamekuwa wakiingia kutoka wilaya ya Aru mkoani Orintale [...]

28/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laangazia ushirikiano wa UM na Muungano wa nchi za Kiislamu

Kusikiliza / Katibu Mkuu  Ban Ki-moon akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao cha ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Nchi za Kiislamu, OIC. Joshua Mmali amekifuatilia kikao hicho: Kikao cha leo katika Baraza la Usalama kimehudhuriwa na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, na Katibu Mkuu wa [...]

28/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani shambulizi liliouwa makumi ya raia Afghanistan

Kusikiliza / Ján Kubiš

  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulio lililofanywa jana jimboni Ghazni ambapo kifaa kilicholipuka kilisababisha vifo vya watu 19 na majeruhi waliokuwa wakisafiri katika bus dogo ambapo waliouwawa ni pamoja na wanawake 16 na watoto kadhaa. Grace Kaneiya na taarifa kamili Mkuu wa UNAMA Ján Kubiš amesema tukio la jana ni [...]

28/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kongamano kuhusu zao la mpunga lataka uwekezaji zaidi Afrika

Kusikiliza / Zao la mpunga

  Kongamano kubwa zaidi barani Afrika juu ya zao la mpunga likihusisha wataalamu, watunga sera na wawakilishi wa wakulima limemalizika huko Cameroon na kutaka Shirika la Chakula na kilimo duniani, FAO kuchochea uwekezaji zaidi unaonufaisha wakulima wadogo. Taarifa zaidi na George Njogopa. (Ripoti ya George) Kongamano hilo la Tatu limehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 650 [...]

28/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maonyesho ya nchi za Kusini yaanza Nairobi:

Kusikiliza / UNEP SOUTH

Maonyesho ya wiki moja ya miradi na mbinu za maendeleo zinazojali mazingira yameanza mjini Nairobi, Kenya yakihusisha nchi zinazoendelea. Maonyesho hayo yameandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia ushirikiano wa nchi zinazoendelea, SOUTH-SOUTH yanafanyika wakati huu ambapo uchumi wa nchi hizo unachangia asilimia 47 kwenye biashara ya dunia. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. [...]

28/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031