Nyumbani » 25/10/2013 Entries posted on “Oktoba 25th, 2013”

Vikosi vya serikali na waasi wa M23 wanapambana huko Goma: Baraza la usalama lataka uchunguzi

Kusikiliza / Askari wa MONUSCO wakiwa kwenye doria huko Goma

Mapema hii leo huko Goma, Mashariki mwa DR Congo kumeibuka mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, mapambano yanayoripotiwa kuhusisha matumizi ya silaha nzito ikiwemo makombora. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amewaambia waandishi wa habari kuwa mapigano bado yanaendelea huko Kibaya kwenye viunga vya mji wa Kibumba kilometa 15 kutoka [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutafungua ofisi Misri kusaidia mchakato wa katiba: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Umoja wa Mataifa unatarajia kufungua ofisi ya kanda nchini Misri kwa ajili ya kusaidia nchi hiyo katika machakato wa kuandika katiba. Katika mahojiano maalum na Dob Bob wa idhaa ya Kingereza ya radio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navy Pillay amesema bado hali ya usalama ni tete [...]

25/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dokta Mukwege atumia uwezo wake wote kurejesha utu na heshima ya wahanga wa ubakaji Mashariki mwa DR Congo

Kusikiliza / Dokta Denis Mukwege

Denis Mukwege, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa zaidi ya takribani miaka 15 amejitolea maisha yake kuokoa wahanga wa ubakaji huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. Akihudumia kwenye hospitali ya Panzi huko Bukavu, hospitali aliyoianzisha mwaka 1993, Dkt. Mukwege na wenzake wametoa usaidizi wa kitabibu kwa maelfu ya wanawake waliokumbwa na [...]

25/10/2013 | Jamii: Makala za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 46.8 zahitajika kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi ufilipino: OCHA

Kusikiliza / Philippines-BoholEQ-diary-lead

Mashirika ya misaada yametoa ombi maalum la dola Milioni 46.8 kusaidia maelfu ya wahanga wa tetemeko la ardhi lililokumba Ufilipino siku Kumi zilizopita. Tetemeko hilo kwenye kisiwa cha Bohol lilisababisha vifo vya watu 201 huku zaidi ya Laki Tatu wakipoteza makazi au kulazimika kuhama ambapo msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada, [...]

25/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takriban watu milioni 2.5 hawajaweza kufikiwa na misaada Syria: OCHA

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA Bi. Valerie Amos akihutubia Baraza la Usalama mjini New York

Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na mashirika ya kibinadamu kuwafikishia misaada watu waloathiriwa na mzozo wa Syria, bado misaada hiyo inayotolewa ni haba mno, na haiwezi kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo.   Bi Amos amesema, [...]

25/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wa Madagascar wahimizwa kudumisha amani wanapohitimisha uchaguzi

Kusikiliza / Wananchi wa Madagascar wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura

Wananchi wa Madagascar wamejitokeza kwa wingi leo kupiga kura kumchagua rais mpya, kwa mara ya kwanza tangu kupinduliwa utaratibu wa kikatiba nchini humo zaidi ya miaka mine ilopita. Jason Nyakundi ya na taarifa kamili: TAARIFA YA JASON Raia wa Madagascar wamekuwa wakipanga foleni ndefu kumchagua rais mpya kwa mara ya kwanza tangu alipopinduliwa Rais Marc [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watoto kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio nchini Syria

Kusikiliza / polioday

Huku Syria ikisubiri kuthibitishwa kwa kesi za ugonjwa wa polio mashariki mwa nchi shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limejiunga na Shirika la afya duniani WHO na washirika wengine katika kuongoza zoezi kubwa la utoaji wa chanjo kwa lengo la kuwakinga watoto nchini humo na eneo lote dhidi ya ugonjwa wa polio. [...]

25/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM yaandaa kongamano kuhusu uhamiaji nchi nne Kusini mwa Amerika

Kusikiliza / iom logo

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Peru juma hili liliwaalika wataalamu wa masuala ya takwimu za uhamiaji kutoka jamii ya Andean kujaribu kubaini jinsi takwimu za uhamiaji zinaweza kuboresha uhamiaji katika eneo hilo. IOM iliwaleta pamoja wataalamu wa masuala ya uhamiaji pamoja na maafisa wengine kutoka wizara za masuala ya kigeni kutoka Bolivia, Colombia, [...]

25/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

NEPAD ndio muarobaini wa maendeleo barani Afrika: Baraza Kuu

Kusikiliza / NEPAD inatekeleza miradi ya kilimo ya kuongeza uhakika wa chakula

Wiki ya Afrika katika Umoja wa Mataifa imefikia kilele Ijumaa kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kujadili mpango mpya wa ushirikiano wa maendeleo barani humo, NEPAD wakimulika zaidi mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake na jinsi ya kuimarisha ushirikiano huo. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Mjadala wa wazi kuhusu NEPAD na [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulinzi wa wanawake vitani ni lazima: Dokta Mukwege

Kusikiliza / Dokta Dennis Mukwege

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake anayejitolea kutibu wanawake waliokumbwa na ubakaji na ukatili wa kingono huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, Denis Mukwege amesema jumuiya ya kimatifa lazima iheshimu na kutoa ulinzi kwa wanawake katika migogoro kwani hudhalilishwa kinyume na hadhi yao katik jamii. Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa hii Dokta Mukwege [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto bado watumiwa vitani DRC

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo yenye migogoro Leila Zerrougui amesikitishwa na matokeo ya utafifi uliotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo, DRC,MONUSCO unaoonyesha kwamba vitendo vya watoto kuhusihwa katika vita na vikundi vyenye silaha nchini humo ni mfumo [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumekosekana chombo cha kumulika maslahi ya wahamiaji:Crépeau

Kusikiliza / Francois Crépeau

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za wahamiaji François Crépeau ameonya juu ya kukosekana kwa chombo maalumu ndani ya Umoja huo ama kwingineko kwa ajili ya kuangazia maslahi ya wahamiaji akisema kuwa hali hiyo ni hatari kubwa. Katika ripoti yake aliyoiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mtaalamu huyo amesema [...]

25/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majaji ICC watoa mwongozo kuhusu kesi ya Ruto na mwenzake

Kusikiliza / William Ruto

Majaji wanaohusika na rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC, wamekataa ombi la makamu wa rais wa Kenya, William Ruto, la kutaka kuruhusiwa kutohudhuria vikao vya kesi inayomkabili. Pia majaji hao wametasfiri vifungu vya sheria vinavyoweza kutoa ruhusa kwa mshtakiwa kutokuwepo mahakani wakati wa kesi yake. Taarifa zaidi na George Njogopa Ruto  anayeshtakiwa [...]

25/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031