Nyumbani » 24/10/2013 Entries posted on “Oktoba 24th, 2013”

Wananchi wafurahia uwepo wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Walinda amani wa UM

Wakati leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa , chombo ambacho ni kiranja wa mataifa mbalimbali 193 kote duniani, kikiongoza katika nyanja za uchumi, siasa na kijamii, kauli mbalimbali zimetolewa kuchagiza umuhimu wa umoja huo. Wananchi wa Afrika mashariki wanazungumziaje umuhimu wa mchango wa Umoja wa Mataifa? Tuanzie nchini Kenya.    

24/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hali ya Abyei yatia wasiwasi: Baraza la Usalama:

Kusikiliza / Balozi Agshin Mehdiyev

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mashauriano ya faragha kuhusu Sudan na Sudan Kusini ambapo wajumbe wameeleza wasiwasi wao juu ya ongezeko la mvutano huko Abyei. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mashauriano hayo, Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba Balozi Agshin Mehdiyev kutoka Azerbajian amesema wajumbe wametaka kila [...]

24/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM Tanzania waeleza jinsi miradi ya vijijini ilivyoboresha maisha

Kusikiliza / un_wash_01

Miradi tunayotekeleza vijijini nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa na imedhihirisha kuwa msingi wa maendeleo ni vijijini kwani zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wanaishi huko. Ni kauli ya  Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou aliyotoa kwenye mahojiano maalum na idhaa hii wakati wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa. Amesema [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni lazima tukuze viwanda na biashara kuinua uchumi wa Afrika :AU

Kusikiliza / Nembo muungano wa Afrika

Wakati wiki ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa ikiendelea mjini New York mwangalizi wa kudumu wa Ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Tete Antonio amesema ili kufikia malengo ya kiuchumi ni lazima bara hilo libadilishe mfumo na kukuza viwanda na biashara. Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa [...]

24/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chanjo za dharura zapangwa dhidi ya uwezekano wa kuwepo mkurupuko wa Polio Syria

Kusikiliza / syria polio

Tangu mkakati wa kimataifa wa kutokomeza polio ulipozinduliwa mnamo mwaka 1988, idadi ya visa vya ugonjwa huo wa kupooza imepungua kwa asilimia 99. Kwa sasa, kuna nchi tatu tu ambazo bado zina ugonjwa huo wa polio, ambazo ni Nigeria, Pakistan na Afghanistan. Wataalamu wanatumai kuwa katika miaka michache ijayo, ugonjwa huo utakuwa umetokomezwa kabisa. Hata [...]

24/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuibuka malaria isotibika ni jambo la kutia hofu: WHO

Kusikiliza / malaria

Shirika la Afya Duniani, WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa aina ya ugonjwa wa malaria ambao hautibiki kwa dawa za malaria zilizopo, na kusema kuwa hali hiyo inazua changamoto kwa juhudi za kuzuia na kutokomeza malaria, na hivyo inapaswa kukabiliwa kama jambo la dharura. Joshua Mmali ana taarifa kamili. (TAARIFA YA JOSHUA) Aina ya ugonjwa wa [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali tambueni jukumu la malezi linalofanywa na wanawake

Kusikiliza / Magdalena Sepulveda

Imeelezwa kuwa majukumu yanayofanywa na wanawake majumbani bila malipo yoyote kama vile kupika, usafi malezi ya watoto na hata watu wazima yamekuwa yakiwaengua wanawake katika mfumo wa kijamii pindi yanapokuwa hayatambuliwi. Kauli hiyo ni ya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini wa kupindukia Magdalena Sepúlveda ambaye amesema kuwa malezi yanapaswa kuwa jukumu la pamoja [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Alberic Kacou, Mwakilishi Mkazi wa UM Tanzania akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kagasheki kwenye maonyesho ya UM jijini DSM

Nchini Tanzania, kilele cha wiki ya Afrika na Umoja wa Mataifa kimeshuhudia hii leo jijini DSM kama anavyoripoti mwandishi wetu George Njogopa. (Ripoti ya George)  Akizungumza wakati wa kilele cha madhimisho hayo, Mwakilishi Mkazi  wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou alisema kuwa ni fahari ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hii wakati dunia ikipiga [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamishna ya fidia ya UM yakamilisha kulipa dola milioni 1.24 kwa Kuwait

Kusikiliza / Ramana ya Kuwait

Kamishna ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utoaji fidia leo imetangaza kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 1.24 kwa serikali ya Kuwait ikiwa na sehemu iliyosalia baada ya kufanyika malipo ya awali katika siku za nyuma. Kamishna hiyo ya utoaji fidia ilianzishwa mwaka 1991 kwa kufuata azimio la baraza la usalama la Umoja [...]

24/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasafirisha misaada ya madawa na chakula kwa watoto nchini Syria

Kusikiliza / UNICEF yawasilisha msaada Syria

Ndege iliyokodishwa  na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF inayobeba madawa yanayohitajika kwa dharura nchini Syria na chakula cha wototo  imewasili mjin iBeirut ambapo misaada hiyo itasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda Syria. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (Taarifa ya Jason) Ndege hiyo ilibeba karibu tani 28.6 za misaada  ya chakula ma [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahofia ghasia kati ya serikali na Renamo huko Msumbiji

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Kuongezeka kwa ghasia kati ya vikosi vya serikali na wafuasi wa chama cha RENAMO nchini Msumbiji kunazidi kumtia hofu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye katika taarifa amenukuliwa akitaka pande zote kujizuia kufanya vitendo vyovyote vinavyoweza kutishia amani. Amerejea makubaliano ya Roma ya mwaka 1992 ambayo amesema yameleta amani iliyodumu kwa miaka 21 [...]

24/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa: Ban ataka ushirikiano zaidi wa kimataifa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akiwa Times Square ambapo kulikuwa na shughuli maalum ya kuadhimisha siku ya UM

Siku ya Umoja wa Mataifa leo 24 Oktoba ambapo kauli mbali mbali zimetolewa kukumbusha jukumu la chombo hicho adhimu chenye wanachama 193. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.  (Taarifa ya Assumpta)  John Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake amesema wakati huu ambapo dunia inahaha kukabiliana na migogoro maeneo mbali [...]

24/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930