Nyumbani » 23/10/2013 Entries posted on “Oktoba 23rd, 2013”

Baraza la usalama lalaani shambulio nchini Mali

Kusikiliza / Mali

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio ililofanywa na kundi lenye silaha lisilofahamika dhidi ya  askari walinda amani chini Mali katika kizuizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani nchini Mali MINUSMA, na kusababisha vifo vya askari kadhaa raia wa Chad na raia wengine kufa na kujeruhiwa. Katika taarifa yake  kwa [...]

23/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tumejizatiti kutokomeza kemikali chafuzi: Tanzania

Kusikiliza / Mafunzo kuhusu kemikali

Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi imependekeza kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu. Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo kemikali hizo ni PCN na HCBD ambapo kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na nchi zinazoendelea kujihami dhidi [...]

23/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ripoti za APRM zinatia matumaini changamoto ni utekelezaji: Balozi Ndangiza

Kusikiliza / Fatuma Ndangiza

Wiki ya Afrika ndani ya Umoja wa Mataifa inaendelea kwenye mjini New York, ambapo Makamu Mwenyekiti wa jopo la watu mashuhuri linalosimamia mpango wa Afrika wa kujitathmini wenyewe, Balozi Fatuma Ndangiza amesema ripoti za tathmini ni nzuri lakini kitendawili ni utekelezaji. Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki kando mwa mkutano na waandishi wa habari, [...]

23/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu Tanzania ni kubwa kuliko makadirio: Dkt. Kamara

Kusikiliza / Moja ya kampeni dhidi ya Kifua Kikuu nchini Tanzania

Ripoti mpya ya WHO kuhusu ugonjwa Kifua Kikuu iliyotolewa Jumatano imeonya uwezekano wa kutoweka mafanikio yaliyopatikana kwenye tiba dhidi ya ugonjwa huo. Hofu hiyo inatokana na uwezekano wa wagonjwa Milioni Tatu duniani kote kuwa nje ya mifumo ya tiba na janga la Kifua Kikuu sugu kuendelea. NchiniTanzaniamafanikio  yaliyopatikana ni pamoja na kupungua kwa maambukizi mapya [...]

23/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizozo inapoaathiri maendeleo, fursa za ukuaji huwepo pia: UNDP

Kusikiliza / Nembo ya UNDP

Licha ya hatua zilizopigwa katika kuzuia migogoro na majanga mwaka ulopita, nchi nyingi bado zinakumbana na migogoro ya mara kwa mara na aghalabu husalia kwenye lindi la umaskini, imesema ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP. Ripoti hiyo ambayo imetolewa wiki hii, inabainisha hatua za ufanisi zilizopigwa na UNDP katika kuzuia na kukabiliana [...]

23/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulizi dhidi ya askari walinda amani Mali

Kusikiliza / Askari mlinda amani,MINUSMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya askari walinda amani chini Mali katika kizuizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani nchini Mali MINUSMA, na kusababisha vifo vya askari kadhaa raia wa Chad na raia wengine kujeruhiwa.  Katika taarifa yake  kwa waaandishi wa [...]

23/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Miradi isiyoharibu mazingira ni gharama lakini ni endelevu: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akizungumza kwenye mkutano huko Copenhagen, Denmark

Uchangiaji fedha kwa ajili ya miradi inayojali mazingira ni kitovu cha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wakati akifungua mkutano kuhusu uchangishaji fedha kwa miradi ya aina hiyo huko Copenhagen,Denmark.  Ban amesema mara nyingi serikali au wawekezaji huona ni gharama kubwa kuwekeza katika miradi inayojali mazingira lakini [...]

23/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM kuhusu haki za wakimbzi wa ndani afanya ziara Serbia na Kosovo

Kusikiliza / Chaloka Beyani

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ameishauri serikali ya Serbia na utawala wa Kosovo kufanya mikakati ya kupata suluhu kwa wakimbizi wa ndani nchini Serbia na Kosovo. Akiongea baada ya kukamilisha ziara rasmi nchini humo Beyani amesema kuwa huu ndio wakati mwafaka wa kupata suluhu. Amesema [...]

23/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mchakato wa UNICEF waendeleza elimu ya watoto wa kike Niger

Kusikiliza / Watoto wasoma chini ya mti

Katika eneo hili la kusini mwa Niger, elimu ya watoto wa kike bado inapata pingamizi kutokana na shinikizo la itikadi za kitamaduni. Asilimia 36 ya wasichana nchini humo huingia ndoa za utotoni kabla ya umri wa miaka 15. Katika kujaribu kupunguza pengo lililopo kati ya watoto wa kike na watot wa kiume wanaokwenda shule, Shirika [...]

23/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Licha ya mafanikio kuna changamoto katika TB; Tanzania tafiti zaibua mapya:

Kusikiliza / Huduma kwa mgonjwa Kifua Kikuu nchini Tanzania

Ripoti iliyochapishwa leo na shirika la afya ulimwenguni WHO imeonyesha mafanikio ya tiba dhidi ya kifua kikuu ikiwemo kuokoa maisha ya watu zaidi ya Milioni 22 duniani kote huku idadi ya wagonjwa ikipungua hadi kufikia watu milioni 8. Mwaka jana. Hata hivyo ripoti hiyo inaonya uwezekano wa kutoweka kwa mafanikio hayo. Grace Kaneiya na taarifa [...]

23/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yachukua tahadhari dhidi ya kemikali chafuzi.

Kusikiliza / Dkt. Julius Ningu, Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania akizungumza kwenye mafunzo hayo

Siku moja baada ya Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi kupendekeza  kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu, serikali ya Tanzania imesema inachukua tahadhari kukabiliana na kemikali hizo kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa viwanda,kilimo na mifugo [...]

23/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laangazia hali ya Darfur na ujumbe wa UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali magharibi mwa Sudan na majukumu ya ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur, UNAMID. Assumpta Massoi na taarifa kamili: TAARIFA YA ASSUMPTA Katika kikao cha leo, Baraza hilo la Usalama limesikiliza ripoti ya Mwakilishi wa Katibu [...]

23/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya CEDAW yaimarisha nafasi ya wanawake katika utatuzi wa migogoro

Kusikiliza / CEDAW-300x266

Nchi ambazo zimesaini mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW zimehimizwa kuhakikisha zinazingatia haki za wanawake wakati na hata baada ya mizozo na pia zinapochangia katika ulinzi wa amani. Alice Kariuki na ripoti kamili. (Ripoti ya Alice) Maelekezo hayo yamo kwenye nyaraka ya aina yake iliyopitishwa na Kamati inayosimamia [...]

23/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Biashara haramu ya mbao Bonde la mto Congo yapatiwa muarobaini

Kusikiliza / Msitu wa bonde la Congo

Nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mbao, pamoja na wawakilishi wa sekta hiyo wameridhia makubaliano ya kupambana na biashara haramu ya mbao kwenye bonde la mtoCongo. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kufuatia mkutano wa kimataifa uliofanyika mjini Brazaville. Taarifa ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.    (Taarifa [...]

23/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mafanikio dhidi ya Kifua Kikuu hatarini kutoweka: WHO

Kusikiliza / Mhudumu wa afya nchini Tanzania akikagua daftari la mgonjwa wa Kifua Kikuu

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO inaonya kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kukabiliana na ugonjwa wa Kifua Kikuu yako hatarini kutoweka. Ripoti hiyo inayotokana na taarifa kutoka mataifa 197 na maeneo inataja mambo mawili yanayotia hatarini mafanikio ya tiba iliyookoa maisha ya zaidi ya watu Milioni 22 duniani kote. Mosi ni wagonjwa Milioni Tatu dunini [...]

23/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930