Nyumbani » 22/10/2013 Entries posted on “Oktoba 22nd, 2013”

Jamii asilia zataka kushirikishwa katika mipango ya maendeleo

Kusikiliza / Paul Kanyinke Sena

Wakati mikutano mbalimbali ya jamii za watu asilia ikichukua kasi mjini New York, kilio kikubwa cha jamii hiyo ni namna miradi ya rasilimali asilia inavyoathiri watu hao hususani barani Afrika pamoja na mitizamo hasi ya serikali kwa kundihilo.  Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, [...]

22/10/2013 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Uganda yaweka mfano wa kuigwa, swala la usajili wa watoto

Kusikiliza / Akina mama nje ya hospitali

Zaidi ya nusu ya watoto walio nchi za kusini mwa jangwa la Sahara hawajasajiliwa ikimaanisha hawana vyeti vya kuzaliwa. Hii inawafanya kukosa kupata huduma muhimu za kijamii. Hali hii imepelekea kufanyika kwa mkutano unaowajumuisha washirika kutoka nchi 13 za Afrika. (Makala ya Grace Kaneiya)

22/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UM wavitaka vyama kinzani kusitisha mashambulizi Msumbiji

Kusikiliza / Ramana ya Msumbiji

Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa makini hali ya kuzorota kwa usalama nchini Msumbiji na umetoa wito kwa pande zinazokinzana kusitisha mapigano hima na kuanzisha majadiliano ya kumaliza tofauti ili kujenga demokrasia ya kweli na maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema Umoja [...]

22/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamia ya wasudan kusini warejea Juba: IOM

Kusikiliza / Wasudan kusini wawasili Juba

Jahazi lililokuwa limechukua raia 856 wa Sudan Kusini waliokuwa wakiishi Sudan limetia nanga huko Juba na hivyo kuhitimisha safari ya abiria hao ya siku 17 iliyoanzia mji wa Renk wa jimbo la Upper Nile, kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa miaka kadhaa sasa mpango wa wananchi hao kurejea Sudan Kusini ulikuwa unakwama kwenye mpaka wa kaskazini [...]

22/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wapendekeza kupigwa marufuku kwa aina mbili za kemikali zitumikazo kuhifadhi mbao na kuua wadudu

Kusikiliza / Unyunyuziaji wa dawa shamabani

Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi imependekeza kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu. Taarifa iliyotolewa leo imetaja kemikali hizo aina ya PCN na HCBD kuwa zimekuwa zikitumika viwandani kwa miaka kadhaa sasa lakini zimeripotiwa kuwa na [...]

22/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rekodi ya haki za binadamu Uchina yamulikwa

Kusikiliza / Ramana ya Uchina

Uchina imetetea rekodi yake ya haki za binadamu, wakati wa ukaguaji wake wa pili wa kimataifa katika Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi. Ukaguzi wa rekodi za haki za binadamu za nchi wanachama hufanyika mara moja kila katika miaka mine. Ujumbe wa Uchina wenye watu 43 uliongozwa na Balozi Wu Hailong kutoka Wizara [...]

22/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kuhusu suala la Palestina na amani Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Baraza la Usalama

   Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadilia suala la Palestina na amani Mashariki ya Kati, wakati ambapo harakati za upatanishi na kusaka amani zimeshika kasi.  Joshua Mmali na taarifa kamili(TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Mkutano wa leo wa Baraza la Usalama umehudhuriwa pia na  wawakilishi wa nchi mbali mbali, zikiwemo zile za [...]

22/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ILO, Bangladesh zazindua mpango wa kulinda sekta za viwanda vya nguo

Kusikiliza / Kiwanda cha nguo Bangladesh

Serikali ya Bangladesh kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la ajira, ILO, limezindua mpango wa juhudi za kuboresha usalama sehemu za kazi kwa wafanyakazi wa sekta za viwanda vya nguo nchini humo. Mpango huo unaogharimu dola za kimarekani milioni 242 unalenga katika kupunguza hatari za moto na kuanguka kwa majengo katika viwanda na kuhakikisha haki [...]

22/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rangi za mapambo zenye madini ya risasi zahatarisha maisha ya watoto na wajawazito: UNEP

Kusikiliza / Mtoto akichora akitumia rangi

Zaidi ya miaka 90 tangu mjumuiko wa mataifa kutoa wito wa kupiga marufuku matumizi ya madini ya risasi kwenye rangi za mapambo na licha ya kuwepo kwa njia nyingine za kuboresha rangi hizo bila kutumia risasi, bado yaelezwa kuwa madini hiyo yatumika. Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP linasema kitendo hicho kinaweka hatarini [...]

22/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria inatoa ushirikiano kwenye uteketezaji wa silaha zake za kemikali: Bi.Kaag

Kusikiliza / Sigrid Kaag

Mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na OPCW ya kusimamia uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali nchini Syria, Sigrid Kaag yuko nchini humo kufuatia uteuzi wake hivi karibuni. Taarifa iliyotolewa hii leo imemkariri akisema kuwa changamoto ni kumaliza kazi ndani ya muda uliopangwa ambao ni katikati ya mwaka ujao. Bi. [...]

22/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ombi la ufadhili wa dharura latolewa wakati Mali ikiachwa bila wafadhili

Kusikiliza / Wakazi wa eneo la Sahel

Watu wanaoishi katika eneo la Sahel barani Afrika ni miongoni mwa watu walio hatarini zaidi duniani, na matatizo yanazidi kuibuka mara kwa mara, imesema Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA. OCHA imesema ukosefu wa ufadhili kutoka kwa jamii ya kimataifa ni mojawapo wa sababu kuu ya misaada kutowafikia watu wanaoihitaji [...]

22/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaweza kupunguza usaidizi wa chakula huko DR CONGO

Kusikiliza / Watoto wa shule ni miongoni mwa wanufaika wa misaada ya chakula itolewayo na WFP

Kutokana na uhaba wa fedha Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limelazimika kupunguza huduma zake maeneo kadha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC hata baada ya kuwasaidia watu milioni 3.6 kati ya mwezi Septemba mwaka 2012 na Juni mwaka huu. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (Ripoti ya Assumpta)  WFP inasema kuwa hali hiyo [...]

22/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wakwamisha usambazaji misaada Syria, huku msimu wa baridi kali ukikaribia

Kusikiliza / Watoto nchini Syria wakijihami na baridi

Mzozo unaoendelea nchini Syria unazidi kutatiza jitihada za huduma za kibinadamu wakati msimu wa baridi unapowadia. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa kwa mwaka  hu pekee karibu asilimia 35 ya misaada yake imeendea watu walio kwenye maeneo yaliyo vigumu kufikiwa kamaAleppo, Azzaz na Karameh. Taarifa zaidi na Alice Kariuki.   [...]

22/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubunifu na uwekezaji suluhisho la mabadiliko ya tabianchi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon akiwa Copenhagen, Denmark

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza huko Denmark katika kongamano la tatu la kimataifa kuhusu uchumi unaojali mazingira na kusema kuwa mabadiliko ya tabianchi ni moja ya vitisho vikubwa vya maendeleo endelevu na kwamba iwapo dunia inataka kuwa na matumizi ya nishati safi basi juhudi za pamoja zahitajika zikihusisha serikali, benki za [...]

22/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930