Nyumbani » 18/10/2013 Entries posted on “Oktoba 18th, 2013”

Sheria za kipindi cha mpito ni lazima zizingatie kanuni za kimataifa za haki: Pillay

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay akihutubia Baraza la Usalama kwa njia ya video kutoka Geneva

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema kulinda haki za wanawake katika mazingira ya mizozo bado ni changamoto kubwa. Bi Pillay amesema hayo wakati akilihutubia Baraza la Usalama kwa njia ya video kutoka Geneva, baada ya wanachama wa baraza hilo kupitisha azimio la kuwajumuisha wanawake katika kuzuia na kutatua [...]

18/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban apokea matokeo ya awali Guinea, ataka amani.

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea matokeo ya awali ya uchaguzi wa kisheria nchini uliofanyika tarehe 28 September nchini Guinea, yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo CENI. Katika taarifa yake Bwana Ban ameongeza serikali ya Guinea, taasisi zake na washikadau wote kwa mchango wao kwa taasisi na kwa kufanya uchaguzi. [...]

18/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Harakati za kutokomeza umaskini Tanzania zamulikwa

Kusikiliza / Soko la nguo za mitumba

Wiki hii Mataifa mbali mbali duniani yaliadhimisha siku ya kutokomeza umaskini ambapo ilielezwa kuwa idadi ya watu maskini inapungua lakini bado watu Bilioni Moja nukta mbili ni mafukara. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alieleza bayana kuwa kupungua kwa idadi hiyo kusipofushe watu macho na kuacha harakati za kuweka mazingira sawia kwa kila [...]

18/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uongozi wa wanawake ni muhimu katika kuendeleza amani: UN Women

Kusikiliza / Phumzile Mlambo-Ngcuka,UN Women

Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka, amekaribisha hatua ya Baraza la Usalama kupitisha azimio la kuongeza nafasi za mchango wa wanawake katika kuzuia na kutatua mizozo, pamoja na kuendeleza amani. Azimio hilo ambalo limepitishwa katika kikao maalum mnamo Oktoba 18, linatoa pia wito wa kuchukuliwa hatua mathubuti [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia ripoti kuwa Saudi Arabia 'imekataa' ujumbe kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Bado sijapokea taarifa rasmi kuhusu ripoti za Saudi Arabia kukataa ujumbe usio wa kudumu kwenye baraza la usalama. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyotoa mchana huu alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na sualahilolililoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari. Bwana Ban amesema ujumbe ndani ya Baraza la Usalama [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laazimia kutambua umuhimu wa wanawake katika kuendeleza amani

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo katika kikao maalumu limepitisha azimio la kuutambua umuhimu wa wanawake katika kuzuia na kutatua mizozo, pamoja na kuendeleza amani. Grace Kaneiya ana ripoti kamili. (Taarifa ya Grace Kaneiya) Azimio la kuutambua mchango wa wanawake limepitishwa katika wakati Baraza la Usalama likikutana kujadili suala la wanaw ake, uongozi [...]

18/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM, EU zapinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu

Kusikiliza / Usafirishaji wa binadamu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaungana na nchi za Jumuiya ya Ulaya na washirika wake kwenye ukanda huo kwenye maadhimisho ya saba ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Biashara hiyo haramu ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya mihadarati ni miongoni mwa changamoto kubwa za ukiukwaji wa haki za binadamu na huhusisha [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yataka kukomeshwa kwa madini ya risasi za kuta kuwalinda watoto

Kusikiliza / rangi

Shirika la afya ulimwenguni WHO limeanzisha juhudi za kukomeshwa kwa uzalishaji na matumizi ya rangi za kung'arisha ikiwemo kuta na wanasesere ambazo zina madini ya risasi kwa kuwa imebainika kuwa na athari kubwa kwa afya za watoto hasa kwenye ubongo wao. George Njogopa na ripoti kamili (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) WHO inasema kuwa zaidi ya asilimia [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa Corona waibuka Mashariki ya kati

Kusikiliza / Madakatari waangalia picha za x-ray

Shirika la afya ulimwenguni WHO limefahamishwa kuhusiana kuzuka kwa ugonjwa wa matatizo ya kupumua unaosababishwa na virusi vya Corona ambao umeikumba nchi ya Qatar. Tayari mtu mmoja mwenye umri wa miaka 61 ambaye amekubwa na tatizo hilo amelazwa katika hospitali moja tangu Oktoba 11 akipatiwa matibabu ya karibu. Vipimo vilivyochukuliwa na baadaye kujaribiwa katika maabara [...]

18/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto 7 kati ya 10 CAR hawajarejea shuleni:UNICEF

Kusikiliza / Watoto nchini CAR

Watoto saba kati ya watoto 10 walio na umri  wa kwenda shuleni kwenye Jamhuri yaAfricaya kati hawajarejea shuleni tangu kuanza kwa mzozo mwezi Disemba mwaka 2012. Jason Nyakundi na taarifa kamili.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)  Karibu asilimia 65 ya shule zilizokaguliwa zimeporwa au zimeharibiwa na risasi au mabomu. Wanne kati ya watu watano wanasema kuwa [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yazitaka nchi kufungua mipaka na kuruhusu kupita kwa wakimbizi kutoka Syria

Kusikiliza / Wahamiaji wa kutoka Syria

Huku idadi ya raia wa Syria wanaotafuta hifadhi barani Ulaya ikizidi kuongezeka, Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na changamoto wanazopitia wakati ya safari zao. Alicekariuki na maelezo zaidi.  (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Hii ni pamoja na matukio ya kushamgaza ya mamia ya Wasyria wanaozama baharini. Shirika la [...]

18/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria za kutetea watoto bado zina ubaguzi dhidi ya watoto wa kike: Ripoti

Kusikiliza / Marta Santos Pais

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupinga ukatili dhidi ya watoto Marta Santos Pais amesema licha ya serikali kupitisha sera na sheria za kupinga vitendo hivyo, bado kuna ubaguzi wa jinsi ambavyo sheria hizo zinatetea kundi hilo.  Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu ripoti aliyowasilisha mbele [...]

18/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031