Nyumbani » 14/10/2013 Entries posted on “Oktoba 14th, 2013”

Tuendeleze azma ya Mwalimu ya kupata suluhu bila kumwaga damu: India

Kusikiliza / Balozi Asoke Kumar Mukerj.jpg

Ni jambo la muhimu sana kutambua kuwa uhuru wa iliyokuwa Tanganyika kama ilivyokuwa kwa India ulipatikana bila kumwaga damu, na hiyo ni jambo la kujifunza jinsi Mwalimu Nyerere alivyoweza kushawishi kupitia mashauriano na mazungumzo hadi nchi yake kupata uhuru. Ni kauli ya Mwakilishi wa Kudumu wa India kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Asoke Kumar Mukerji [...]

14/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nyerere alitufundisha kuthamini uhuru: Mwakilishi wa Afrika Kusini

Kusikiliza / Kingsley Mamabolo

Katika kumkumbuka Mwalimu Julius Nyerere mnamo Oktoba 14, Mwakilishi wa Kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa, Kingsley Mamabolo, amesema kuwa Mwalimu Julius Nyerere alitoa mafunzo muhimu kwa wanadamu kufurahia na kuthamini uhuru daima. Akisifu mchango wake kwa ukombozi wa Afrika Kusini kutokana na uongozi wa ubaguzi wa rangi na kwa makundi mengine ya [...]

14/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nyerere ni dira ya dunia: Watanzania

Kusikiliza / Nyerere

Baadhi ya wananchi waTanzania waliohudhuria hafla ya kwanza ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu kifo cha mwasisi wa taifa hilo marehemu Julius Nyerere wamesema kiongozi huyo ataendelea kubakia lama ya umoja,maendeleo na hata ukombozi wa elimu Afrika na duniani.  Wakiongea katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii wananchi hao wamesema kiongozi huyo alitamka mambo [...]

14/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi wa ukombozi wa Afrika: Mwakilishi wa AU

Kusikiliza / Antonio Tete

  Mwangalizi wa Kudumu wa Muungano wa Nchi za Afrika kwenye UMoja wa Mataifa, Antonio Tete, amemtaja Hayati Mwalimu Julius Nyerere kama mtu anayekumbukwa kama kiongozi wa ukombozi wa Afrika. Akiongea wakati wa kuadhimisha Siku ya Mwalimu Julius Nyerere, ambayo imeadhimishwa kwa mara ya kwanza kwenye Umoja wa Mataifa, Bwana Tete amemsifu Mwalimu Nyerere kama [...]

14/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uadilifu na ujasiri wa Mwalimu Nyerere ulitupa mwongozo: Eliasson

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amesema kuwa itikadi, uadilifu na ujasiri wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere uliwapa wengi msukumo na mwongozo wa kutenda wema. Bwana Eliasson ambaye amekuwa mgeni wa heshima kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mwalimu Nyerere, Oktoba 14, ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya kifo chake, amesema [...]

14/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nyerere akumbukwa kwa kuunganisha watanzania:Shairi

Kusikiliza / Wakati akighaini shairi kumuenzi Mwalimu Nyerere,Haji Khamis

Katika tukio la kumuenzi Baba wa Taifa la Tanzania lililofanyika Umoja wa Mataifa mjini New York, siku ambayo pia ni kumbukumbu ya kifo chake miaka 14 iliyopita, mwakilishi wa Jumuiya watanzania mjini humo Haji Khamis alighani shairi kuhusu maisha ya mwalimu na mchango wake kwa Tanzania. Na alianza kwa salamu… (Shairi Haji)

14/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nyerere amechangia pakubwa ukuaji wa Kiswahili duniani:Balozi Macharia

Kusikiliza / Balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Macharia Kamau

Lugha ya Kiswahili imepata umaarufu mkubwa duniani na inaendelea kukua hadi sasa kwa ajili ya mchango mkubwa wa baba wa taifa la Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hayo yamesemwa na balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Macharia Kamau wakati wa hafla maalumu ya kumuenzi mpigania uhuru huyo kwa mara ya kwanza kwenye Umoja wa [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwalimu Nyerere miaka 14 baada ya kifo chake, fikra zake zazidi kuchanua

Kusikiliza / Assumpta Massoi, Profesa Ali Mazrui na Flora Nducha

Julius Nyerere, Jabali wa Afrika- Mitizamo toka Arusha hadi Obama, kitabu kilichoandikwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Profesa Linda Mhando. Je nini hasa lengo la kuandika kitabu hiki? Flora Nducha na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na Profesa Mazrui ambaye alikuwepo katika siku maalum ya kumuenzi [...]

14/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchango wa mwalimu Nyerere asilani hautosahaulika:Linda Mhando

Kusikiliza / Linda na Flora

Mwanzilishi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere ambaye ameenziwa kwa mara ya kwanza kwenye Umoja wa Mataifa mwaka huu Oktoba 14, amemiminiwa sifa lukuki na watu mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa kitabu "Julius Nyerere jabali wa Afrika kutoka azimio la Arusha hadi Obama. Kitabu hicho kimehaririwa na Profesa Ali Mazrui kutoka Kenya na profesa Linda [...]

14/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Aliyoyatetea Mwalimu Nyerere yako dhahiri hadi sasa: Jamaica

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu, UM wa Jamaica Courtenay Rattray

Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi mwenye dira na yale aliyoyatetea tunayashuhudia sasa na tunayapigia chepuo katika ajenda ya baada ya mwaka 2015, ni kauli ya mwakilishi wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa wa Jamaica Courtenay Rattray aliyotoa wakati akihutubia kwenye tukio maalum la Kumuenzi Baba wa Taifa la Tanzania kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani kuongezeka kwa mashambulizi ya bomu Iraq

Kusikiliza / Ramana ya Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa BanKi-moon amelaani vikali msururu wa mabomu ambayo yamewaua na kuwajeruhi watu wengi katika siku chache zilizopita nchini Iraq, wakiwemo wanafunzi wa shule. Bwana Ban ametuma risala za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali ya Iraq, huku akiwatakia majeruhi nafuu haraka. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu [...]

14/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Profesa Mazrui azungumzia UM kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere

Kusikiliza / Profesa Ali Mazrui

Wakati Umoja wa Mataifa ukitumia siku yale kumkumbuka Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Nyerere, Profesa Ali Mazrui ambaye naye anahudhuria tukio hilo amelizungumzia na kusema ni kitendo sahihi kwa kuzingatia kuwa Tanganyika kabla ya uhuru ilikuwa chini ya uangalizi wa baraza la wadhamini. Profesa Mazrui amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii, [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuboreshwa kwa teknolojia kunaweza kuokoa maisha kupotea majanga kwa mujibu wa ripoti wa shirika mwezi mwekundu

Kusikiliza / Nembo ya IFRC

Kutokuwepo uwezo wa kupata habari na ukosefu wa teknolojia kumekuwa na athari kubwa kwa uwezo wa watu kujiandaa na kurejea hali yao ya kawaida baada ya kutokea kwa majanga kwa mujibu wa ripoti kuhusu majanga ya mwaka 2013 iliyotolewa na shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na lile na mwezi mwekundu. Ripoti ya mwaka huu [...]

14/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kunahitajika uwekezaji zaidi wa kifedha kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi-Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea mwito Jumuiya ya Kimataifa kuwekeza zaidi katika teknolojia ya vyombo vya fedha ili kukabiliana na tabia ya mabadiliko ya tabia nchi akisema kuwa wakati unakimbia kukabilia changamoto zizotokana na mabaidiko hayo. Akisisitiza zaidi, Ban amezitaka jumuiya hizo kuowanisha mifumo ya kisera pamoja na mienendo ya ufanyaji [...]

14/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lasikiliza ripoti za mahakama za kimataifa za Rwanda na Yugoslavia

Kusikiliza / ictr

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeombwa kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ICTR ili kuwapokea washukiwa waloachiliwa na wale ambao hawakupatikana na hatia, kama sehemu ya kuwahamisha kwa ajili ya usalama wao. Joshua Mmali ana maelezo zaidi   TAARIFA YA JOSHUA   Ombi hilo la mahakama ya ICTR, limewasilishwa [...]

14/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

GAVI kuwachanja watoto milioni 250 ifikapo kwaka 2015

Kusikiliza / chanjo

Ripoti mpya iliyotolewa inaonyeha kuwa ubia wa chanjo duniani GAVI uko kwenye mkondo kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwachanja karibu watoto milioni 250 ifikapo mwaka 2015 ambapo vifo milioni moja vitazuiwa kwenye mpango huo. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (Taarifa ya Jason) Kwenye ripoti ya GAVI iliyochapishwa hii leo inasema kuwa watoto wengi zaidi wanafikiwa na chanjo [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yatosha sasa ajali hizi za wahamiaji-IOM

Kusikiliza / jumber-omari-jumbe3-100x86

 Kufuatia ajali ya pili mfululizo ya boti iliyohusisha wahamiaji nchini Italia na kusababaisha vifo vya watu wapatao 34, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limealaani hatua hiyo na kusisitiza wito wao wa kuzitaka nchi za Ulaya kuepusha majanga hayo.  Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema [...]

14/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Katika siku ya kupunguza majanga dunia, UM wawaangazia watu wenye ulemavu

Kusikiliza / disabilities2

Katika kilele cha kuadhimisha siku za kupunguza majanga duniani, inayoadhimishwa kila Oktoba 13,Umoja wa Mataifa umezitolea wito nchi wanachama kuhakikisha zinatoa usalama kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kuwashirikisha katika mipango pamoja na dhana za uokoji. Katika ujumbe wake siku hiyo, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema kuwa jambo linalopaswa kuzingatiwa ni kuhakikisha kwamba mifumo yote ya [...]

14/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wamkumbuka Hayati Mwalimu Nyerere

Kusikiliza / Julius Kambarage Nyerere

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo, shughuli maalum inafanyika kumkumbuka Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tukio linaloenda pamoja na uzinduzi wa kitabu kuhusu jabali huyo wa Afrika, Ripoti ya Assumpta Massoi inaeleza zaidi. (Ripoti ya Assumpta) Miaka 14 tangu kifo chake Hayati Mwalimu Nyerere bado anakumbukwa kwa [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani vikali kushambuliwa kwa kambi ya wakimbizi

Kusikiliza / UNRWA-logo

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limelaani vikali machafuko yaliyozuka katika kambi ya Dera'a iliyoko Kusini mwa Syria ambako wakimbizi kadhaa wameripotiwa kufariki dunia na pia wafanyakazi wa shirika hilo wamejeruhiwa. George Njogopa na ripoti kamili. (Ripoti ya George) Machafuko yaliyoibuka Oktoba 12, mwaka huu yanadaiwa [...]

14/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauaji ya walinda amani watatu wa UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatatu lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya msafara wa mpango wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika Darfur UNAMID. Shambuliohilolimekatili maisha ya walinda amani watatu na kujeruhi mmoja, wote wakliwa ni raia waSenegal. Ban ametoa salamu za [...]

14/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031