Nyumbani » 11/10/2013 Entries posted on “Oktoba 11th, 2013”

Baraza la usalama laridhia jopo la pamoja la OPCW-UM nchini Syria, Ban azungumza

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon(picha ya faili)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia jopo la kwanza kabisa la Umoja wa Mataifa na mshindi wa tuzo ya amani ya nobel mwaka huu, OPCW ambalo ni shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali. Jukumu la jopo hilo ni kusimamia kazi ya kuteketeza na kuharibu mpango wa silaha za kemikali wa Syria [...]

11/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IAEA yahitimisha ziara ya kukagua usalama wa nyuklia Marekani

Kusikiliza / Nembo ya IAEA

Timu ya wataalam wa usalama wa nguvu za nyuklia ikiongozwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, imekamilisha leo ziara ya ukaguzi wa usalama wa mitambo ya umma inayotumia nguvu za nyuklia, na ambayo imepewa vibali na mamlaka ya kudhibiti nyuklia hapa Marekani, NRC. Ukaguzi huo wa wiki mbili, ambao umefanywa kufuatia ombi [...]

11/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wasisitiza amani Sudan na Sudan Kusini ili kufanikisha chanjo ya polio

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Sudani na kundi la Sudan People's Liberation Movement-North (SPLM-N kumaliza tofauti zao ili kuwezesha kampeni ya chanjo dhidi ya polio inayotarajiwa kuanza Novemba tano mwaka huu chini ya mashirika matatu ya Umoja huo lile la uratibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada [...]

11/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Elimu kwa watoto wa kike bado changamoto kubwa

Kusikiliza / Watoto wakike darasani

Leo dunia ikiadhimisha siku ya mtoto wa kike kwa kauli mbiu ubunifu katika elimu kwa wasichana , bado elimu ni changamoto kubwa ambapo barani Afrika  na kwingineko wasichana wengi inasemekana wamekosa fursa za elimu kwasababu mbalimbali ikiwamo umaskini na mila potofu.  Noel Thomson wa radio washirika Afya Fm kutoka MwanzaTanzania ametembelea kata ya Isamilo iliyopo mkoani [...]

11/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yajikita katika kuhamasisha unawaji mikono

Kusikiliza / handwashing

Umoja wa Mataifa umeitaja Oktoba 15 kila mwaka kuwa ni siku ya unawaji mikono duniani. Siku hiyo ambayo itaadhimishwa mnamo Jumanne wiki ijayo, iliwekwa ili kukabiliana na matatizo ya kiafya hasa uwezekano wa kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko. Siku hiyo huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali za usafi, ikiwemo kuyashirikisha makundi ya vijana, wanafunzi pamoja na wanaharakati [...]

11/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC Ajenda kuu, mkutano wa wakuu wa AU:Adis Ababa

Kusikiliza / Waziri wa masuala ya kigeni wa Kenya, Amina Mohamed na Grace Kaneiya wa idhaa hii

Mawaziri wa kigeni kutoka nchi mbali mbali walikuwa na mkutano hapa mjini New York ambapo walijadilili maswala mengi likiwemo swala la ICC mmoja wa aliyehudhuria mkutano ni Waziri wa masuala ya kigeni wa Kenya Amina Mohamed  wakati wa ziara yake ya kikazi  mapema mwezi huu alizungumza na Idhaa hii ambapo kwanza nilimuuliza kuhusu Mkutano aliokuwa [...]

11/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nyerere kuenziwa jumatatu kwa tukio maalum New York

Kusikiliza / Msami akimhoji balozi Manongi

Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa hii Joseph Msami amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake wa  kudumu [...]

11/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM yaongeza msaada Ufilipino baada ya kupata dola milioni 1

Kusikiliza / IOM yatoa msaada Ufilipino

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM liameanzisha mikakati ya kutoa misaada maeneo ya Mindanao kusini mwa Ufilipino baada ya kupokea  dola milioni moja kutoka kwa serikali ya Japan. Fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia watu walioathiriwa na  mapigano yaliyotokea kwenye mji wa Zamboanga. Shughuli hiyo itatetekelezwa kupitia ushirikiano na idara ya masuala ya jamii nchini Ufilipino pamoja [...]

11/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu 42 wanyongwa nchini Iraq kwa kipindi cha siku mbili na wengine 400 zaidi kunyongwa

Kusikiliza / Kamishan Mkuu wa haki za binadamu, Navi Pillay

Watu 42 wamenyongwa nchini Iraq  akiwemo mwanamke mmoja kwa kipindi cha siku mbili zilizopita kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Watu hao walinyongwa baada ya  kupatikana na makosa ya kuhusika kwenye vitendo vya ugaidi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Kamishina mkuu wa haki za binadamu [...]

11/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tuwekeze kwa elimu ya watoto wa kike ili waendelee na kutusaidia: Ban

Kusikiliza / Elimu kwwa mtoto wa kike

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amesema kuwapa watoto wa kike uwezo, kuhakikisha haki zao za binadamu na kukabiliana na ubaguzi na ukatili wanaokumbana nao ni muhimu kwa maendeleo ya familia ya ubinadamu. Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Katika [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yazindua kampeni ya kutokomeza matumizi ya zebaki kwenye vifaa vya utabibu

Kusikiliza / Kifaa cha kupima joto kilicho na zebaki

Shirika la afya duniani, WHO limezindua kampeni ya kutokomeza matumizi ya zebaki katika vifaa vya utabibu. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. (Ripoti ya Alice) Kampeni hiyo iitwayo Sekta ya afya bila zebaki ifikapo mwaka 2020 inalenga kuondosha matumizi ya vipimajoto na vipima shinikizo la damu vyenye madini hayo hatarishi. WHO inasema kampeni hiyo itatokomeza [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Nyerere kuadhimishwa Umoja wa Mataifa Jumatatu

Kusikiliza / Mwalimu Julius Nyerere

Kwa mara ya kwanza kumbukumbu ya Baba wa Taifa laTanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itafanyika kwa mara kwanza makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi waTanzaniakatika Umoja wa Mataifa ambapo Mwakilishi wake wa  kudumu Balozi Tuvako Manongi anatoa ufafanuzi.  (Sauti ya Balozi Manongi) Shughuli hiyo itaenda [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Operesheni ya OPCW na UM nchini Syria yaendelea vizuri

Kusikiliza / OPCW

Siku kumi za kwanza za jopo la pamoja la OPCW na Umoja wa Mataifa za kuthibitisha taarifa za mpango wa silaha za kemikali nchini Syria zimeelezwa kuwa za mafanikio. Taarifa kutoka ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa katika kipindi hicho jopo hilo la awali liliweza kukagua maeneo matatu na kwamba mipango inaendelea [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yaipongeza Tunisia kupitisha sheria kutokomeza utesaji:

Kusikiliza / Ramana ya Tunisia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeipongeza serikali ya Tunisia kwa hatua iliyochukua katika kuelekea kutokomeza masuala ya utesaji. Bunge la nchi hiyo limepitisha sheria ambayo itaanzisha shirika litakalokuwa linasimamia utokomezaji wa masuala ya utesaji.  Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamuTunisia imekuwa ni nchi ya kwanza kwa Mashariki ya Kati [...]

11/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waliofariki dunia kwenye ajali ya mashua Lampedusa wafikia 311

Kusikiliza / Boti kama hii ilizama Lampedusa

Imefahamika kuwa zaidi ya wahamiaji 311 walifariki dunia katika ajali ya mashua iliyotokea wiki iliyopita katika kisiwa cha Lampedusa,Italia. George Njogopa na taarifa kamili. (TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imesema kuwa wahamiaji wengine 156 wengi wao wakiwa ni raia wa Eritrea waliokolewa na imeelezea [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OPCW yashinda tuzo ya amani ya Nobel: Ban apongeza

Kusikiliza / Medali ya tuzo ya amani ya Nobel

Shirika la kimataifa la kupinga matumizi ya silaha za kemikali, OPCW limeshinda tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2013. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (Taarifa ya Assumpta) OPCW lilikuwa miongoni mwa majina 259 yaliyowasilishwa kuwania tuzo hiyo ambapo shirika hilo ambalo kwa sasa linasimamia uteketezaji wa mpango wa silaha za kemikali wa [...]

11/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031