Nyumbani » 10/10/2013 Entries posted on “Oktoba 10th, 2013”

ILO yazindua kampeni ya kadi nyekundu kwa ajira za watoto

Kusikiliza / Red_Card_EN

Shirika la Kimataifa la Ajira, ILO, limezindua kampeni ya kusaidia kupiga vita ajira za watoto. Kampeni hiyo iitwayo, Kadi Nyekundu kwa Ajira za Watoto, imezinduliwa wakati wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ajira za watoto, ambalo limehitimishwa leo Oktoba 10 mjini Brasilia, Brazil. Kampeni hiyo inalenga kutoa chagizo kwa umma kuchukua hatua kutokomeza ajira [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban afurahishwa na kuachiwa huru kwa waziri mkuu wa Libya

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amefurahishwa na kuachiwa kwa waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan na kusisitiza uungwaji mkono kwa serikali ya Libya huku akirejelea kulaani utekwaji nyara kwa kiongozi huyo. Katika taarifa yake Bwana Ban amevitaka vyama mbalimbali na watu wa Libya kukubaliana katika vipaumbele vya taifa na kujenga nchi [...]

10/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha mkutano wa kumaliza migogoro Myanmar

Kusikiliza / Wahamijai Mynmar

Umoja wa Mataifa umekaribisha maamuzi ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa makabila yote yenye silaha nchini Myanmar ili kuungana, mkutano ambao unaimarisha tumaini la kumalizika kwa amani kufuatia vita vilivyodumu kwa zaidi ya nusu karne nchini humo na kuanza kwa majadiliano ya kisiasa. Hayo yamebainishwa katika taarifa ya mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja [...]

10/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Majanga yanapotokea,walemavu hupata madhara zaidi: Wahlström

Kusikiliza / Margareta Wahlstrom

Mazingira wanayokumbana nayo walemavu wakati wa kukabiliana na majanga bado si nzuri, amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye utekelezaji wa mkakati wa kupunguza athari za majanga Margareta Wahlström katika maadhimisho ya kimataifa ya siku hiyo tarehe 13 mwezi huu inayomulika zaidi walemavu. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, [...]

10/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Magonjwa ya akili bado yasumbua dunia

Kusikiliza / wagonjwa wa akili

Dunia inapoadhimisha siku ya afya ya akili leo, shirika la afya duniani, WHO linasema wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea ndiyo wanaoshmabuliwa zaidi na magonjwa ya akili.  Mwandishi wetu wa Tanzania George Njogopa anaangazia hali ya ugonjwa ahuo nchini humo ambapo ametembelea hospitali ya taifa ya  Muhimbili jijini Dar es Salaama ili [...]

10/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UM wapigia chapuo elimu ya mtoto wa kike

Kusikiliza / Watoto wa shule Sudan

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu limeanzisha mkakati ambao unazitaka serikali, mashirika ya kirai, sekta binafsi pamoja na watunga sera duniani kutoa kila kinachowezekana kwa watoto wasichana ili kuhakikisha dunia ina maisha bora kupitia elimu. George Njogopa na maelezo kamili TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA) Katika taarifa yao ya pamoja [...]

10/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa vyoo wasababisha utoro wa watoto wa kike shuleni: UNICEF

Kusikiliza / Watoto wa kike katika shule ya sekondari ya juu Shahid Shudorshon nchini Bangladesh

Katika kuelekea siku ya mtoto wa kike duniani  hapo kesho, nchini Bangladesh, ubunifu wa mbinu rahisi na salama umewezesha kurejesha watoto wa kike shuleni ambao awali waliamua kuacha masomo kutokana na  uhaba wa vifaa vya kujisafji pamoja na vyoo. Deepti Rani Devi ambaye ni Mwalimu katika shule hiyo iitwayo Shahid Shudorshon amesema mwaka 2011 walishuhudia [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuongeza usaidizi wa UM kwa CAR

Kusikiliza / Charles-Armel Doubane, Mwakilishi wa kudumu wa CAR katika Umoja wa Mataifa akihutubia Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza nguvu za ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, na usaidizi wa Umoja wa Mataifa kwa taifa hilo. Joshua Mmali na taarifa kamili (RIPOTI YA JOSHUA MMALI) Kwa mujibu wa azimio namba 2021 linaidhinisha kuongeza [...]

10/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mpango wa kushughulikia ubora wa maji wazinduliwa mjini Budapest

Kusikiliza / water3

Katika jitihada za kuboresha usimazizi wa maji duniani Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa ushirikiano na taasisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira na mradi wa kimataifa kuhusu maji wamezindua mpango unahusu viwango vya maji duniani kwenye mkutano kuhusu maji mjini Budapest. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Afya [...]

10/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatma ya watoto wakimbizi wa Syria nchini Jordan mashakani: UNICEF

Kusikiliza / syrian children jordan

Maelfu ya wakimbizi watoto kutoka Syria walioko nchini Jordan wako hatarini kutelekezwa na hata kutumikishwa, hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Inaelezwa kuwa zaidi ya watoto hao 120,000 hawaendi shule ilhali wengine Elfu Thelathini wanatumikishwa katika ajira kama njia mojawapo ya kuwawezesha kukidhi mahitaji yao. UNICEF inasema [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ashutushwa na kutekwa nyara kwa waziri mkuu wa Libya

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ameelezea kustushwa kwake na taarifa za hapo awali kwamba Waziri Mkuu wa Libya , Ali Zeidan, ametekwa nyara na watu watu wenye silaha mjini Tripoli.Akizungumza na waandishi wa habari nchini Brunei Bwana Ban amesema amefanya mawasiliano na mwakilishi wake maalum nchini Libya , Tarek Mitri,ambaye amekuwa [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahimiza kujali maslahi ya wazee kwenye Siku ya Afya ya Akili

Kusikiliza / Mshauri wa afya ya akili akizungumza na wagonjwa DRC

Katika kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani, leo Oktoba 10, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema siku hii inatoa fursa ya kuongeza ufahamu kuhusu matatizo ya afya ya akili wanayokumbana nayo wazee, hususan wenye umri wa miaka zaidi ya 60. Bwana Ban amesema wakati watu wengi hutazamia kuufikia umri wa uzeeni [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za ASEAN zimesonga mbele kutekeleza malengo ya milenia: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM akihutubia kikao cha pamoja cha ASEAN na UM huko Brunei.

Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN umetumia kikao chao cha pamoja kutathmini miaka miwili ya azimio la pamoja kuhusu ubia wao ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema nyaraka hiyo imejenga msingi wa ushirikiano ambao unakua na kuimarika kila siku hususan katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia. Grace [...]

10/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031