Nyumbani » 08/10/2013 Entries posted on “Oktoba 8th, 2013”

Somalia yaendelea kuimarisha taasisi, sasa yamulika kikosi cha zimamoto

Kusikiliza / Mazoezi yakiendelea

Nchini Somalia kazi ya kuimarisha taasisi za umma kama nguzo mojawapo ya kuhakikisha serikali inawajibika ipasavyo inaendelea.  Takribani miezi kumi iliyopita kikosi cha zimamoto kilianzishwa ili kufanya kazi za uokoaji ikiwemo kuzima moto. Changamoto ni stadi kwa watendaji na hilo limepatiwa jawabu na kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM na Umoja wa Mataifa [...]

08/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Cameroon yafanya kampeni ya chanjo kufuatia kuzuka homa ya manjano

Kusikiliza / Mtoto apewa chanjo Cameroon

Serikali ya Cameroon imefanya kampeni ya chanjo ya halaiki na kuwafikia asilimia 94 ya watu wapatao laki sita na elfu sitini na tatu katika wilaya zilizopo kwenye hatari ya maambukizi ya homa ya manjano. Kampeni hiyo ilifanyika kati ya Agosti 27 na Septemba 1 katika eneo la Littoral, kufuatia visa viwili vya homa ya manjano [...]

08/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yakwamua maisha ya wakimbizi wa Burundi wanaorejea makwao

Kusikiliza / Burundian refugees

Miezi tisa baada ya wakimbizi wa Burundi kurejeshwa kwao na serikali ya Tanzania wengi wao wanakumbana na changamoto za kiuchumi katika kutangamana na jamii zao. Wengi wao hawapati huduma za afya, maji, usafi na chakula. Shirika la uhamijai duniani IOM linawasaidia wakimbizi hawa ili kukidhi mahitaji yao kama anavyoeleza msemaji wake Jumbe Omari Jumbe (SAUTI [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongomano kuhusu ajira za watoto laanza Brazil

Kusikiliza / child labor

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ajira za watoto limeanza leo kwenye mji mkuu wa Brazil, Brasilia. Kongamano hilo limeandaliwa na serikali ya Brazil, ambayo imezialika nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kushiriki kwa minajili ya kuongeza juhudi za kimataifa za kupinga ajira za watoto. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Áder wajadili Syria na mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais János Áder wa Hungary

Suala la Syria na mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa ajenda zilizotawala mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Rais wa Hungary János Áder mjini Budapest siku ya Jumanne. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo Bwana Ban amesema wamejadili kazi inayoendelea ya kuharibu silaha za kemikali nchiniSyria, [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kundi la raia wa Sudan Kusin waliokwama Renk sasa waanza kurejeshwa

Kusikiliza / Raia wa Sudan Kusini wrejeshwa nyumbani kwa meli

Meli kubwa ya mzigo ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, imeondoka huko Sudan Kusin ikiwa imechukua wahamiaji 947 waliokuwa wamekwama katika eneo la Renk tangu mwaka 2011. Meli hiyo inatazamiwa kutua nanga katika mji wa Juba katika kipindi cha siku zinazokadiriwa 15 tangu iondoke huko Oktoba 4. Itapowasili Juba, raia hao wanatazamiwa kupatiwa fedha [...]

08/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yakumbwa na ukata kusaidia wakimbizi wa ndani DR Congo

Kusikiliza / Wakimbizi huko DR Congo wakipatiwa misaada na WFP

Kwa mujibu wa tathmini ya awali, Shirika laKimataifa la Mpango wa chakula WFP, linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vitenda kazi ili kukabiliana na matatizo yanayoendelea kujitokeza Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, hatua ambayo imelifanya kuchukua chakula kutoka katika maeneo mengine na kupeleka huko. George Njogopa na maelezo kamili (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)Kwa kuzingatia kiwango [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Karibu nusu ya dunia watakabiliwa na upungufu wa maji 2030:

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa Budapest

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kudhibiti rasilimali muhimu ya maji ni changamoto hasa kutokana na ongezeko la uchafusi wa mazingira na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.Flora Nducha na taarifa kamili (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa maji na usafi mjini Budapest Hungary amesema ifikapo mwaka [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waadhimisha msaada wa dharura kwa waathiriwa na mzozo nchini Ufilipino

Kusikiliza / Ramana ya Ufilipino

Mfuko wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) imetoa dola milioni tatu  zitakazowasidia watu wa Samboanga walio kusini mwa Ufilipino walioathiriwa na mzozo hivi majuzi. Mzozo huo umewalazimisha watu 125,000 kuhama nmakwao nusuyaowakiwa wamechukua hifadhi  kwenye vituo uokoaji. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibiadamu OCHA inasema kuwa nyumba za [...]

08/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tubadili fikra tuweze kufanya biashara miongoni mwetu: Tanzania

Kusikiliza / Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo leo umeingia siku ya pili na mwisho ambapo wajumbe wanajadili jinsi ya kuhakikisha fedha zinapatikana kutekeleza shughuli za maendeleo. Joseph Msami na ripoti kamili.  (Taarifa ya Joseph Msami)  Katika mkutano  huo nchi zinazoendeleaTanzaniaimeeleza kuwa imeweka mikakati ya ndani ya kujipatia fedha za kufadhili [...]

08/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031