Nyumbani » 07/10/2013 Entries posted on “Oktoba 7th, 2013”

Ban asikitishwa na ghasia zilizojiri Misri Jumapili

Kusikiliza / Ramana ya Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameshutumu vikali ghasia zilizoibuka Jumapili nchini Misri wakati wa maandamano na kusabaisha vifo vya watu zaidi ya 50 huku akituma rambirambi kwa wafiwa na kutakia ahueni ya mapema waliojeruhiwa kwenye zahma hiyo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bwana Ban amerejelea wito wa kutaka maandamano [...]

07/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laanza mjadala wa siku mbili kuhusu ufadhili wa maendeleo

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe

Mjadala wa siku mbili wa ngazi ya juu kuhusu ufadhili wa maendeleo umeanza leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York. Kauli mbiu ya mjadala huo ni: Hatua zilizopigwa katika kutekeleza makubaliano ya Monterrey, azimio la Doha kuhusu ufadhili wa maendeleo na matokeo ya mikutano husika ya Umoja wa Mataifa na majukumu [...]

07/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Lengo la sita la maendeleo ya milenia laangaziwa

Kusikiliza / Watu wasubiri kupimwa, Tanzania

Lengo la sita la malengo ya milenia ni kukabiliana na magonjwa ukiwemo Hiv/ Ukimwi Huko Tanzania kumezinduliwa kampeni ya kupimwa kwa hiari basi ungana na Enes Mwaisakila kutoka radio washirika Jogoo Fm, kutoka RuvumaTanzania kujua hali ilivyo.  (Makala ya Enes Mwaisakila)

07/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNECE yatoa ripoti kuhusu changamoto: usimamizi wa makazi na ardhi

Kusikiliza / Makazi, UNECE

Takwimu zilizotolewa na Kamishna ya biashara ya Umoja wa Mataifa kwa Ulaya UNECE zinaonyesha kuwepo kwa tatizo kubwa la ukosefu wa nishati ya umeme kwa baadhi ya nyumba katika nchi za Ulaya na Asia ya Kati. Ripoti ya kamishna hiyo inasema kuwa nyumba nyingi zinazokaliwa na vijana zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati ya [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanachama wa Baraza la Usalama wazuru ukanda wa Maziwa Makuu

Kusikiliza / Wanachama wa Baraza la Usalama wakiwa kambi ya Mugunga karibu na Goma

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamo ziarani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu, ambako tayari wamezuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC na Rwanda, kabla ya kuwasili nchini Uganda. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) Kabla ya kuondoka mjini Goma DRC Jumapili jioni na kuelekea Kigali, Rwanda, wanachama hao wa [...]

07/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Siku ya Makazi duniani yamulika usafiri mijini

Kusikiliza / Leo ni siku ya makazi duniani

Wakati siku ya makazi duniani inaadhimishwa leo na kauli mbiu usafiri mijini, bado hali ya usafiri mijini ni duni hususan kwa nchi zinazoendelea na hivyo kuendelea kukwamisha shughuli za kiuchumi. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (JASON TAARIFA) Usafiri mjini ni jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kw mataifa mengi, kuongezeka kwa vyombo vya usafiri kumechangia [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miongo minne katika kifungo cha kutengwa ni mateso: Mtaalamu,UM

Kusikiliza / Juan Mendez

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya vitendo vya utesaji Juan E. Méndez, ameitaka serikali ya Marekani kuondoa kifungo cha kutengwa alichowekewa Bwana Albert Woodfox  kilichowekwa tangu mwaka 1972. George Njogopa na taarifa kamili. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)  Bwana  Woodfox  pamoja na mwenzake Herman Wallace, walikumbwa na adhabu hiyo baada ya kutiwa hatiana kuhusika [...]

07/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vikundi 130 kutoka Afrika vyataka ICC iungwe mkono

Kusikiliza / Jengo la ICC

Huko Johannesburg, Afrika Kusini vikundi 130 barani Afrika vimeweka hadharani baruayaoinayotaka nchi za barahilozilizo wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC kuunga mkono mahakama hiyo wakati wa kikao maalum cha wakuu wa nchi za Muungano wa Afrika. Kikao hicho kitafanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu hukoAddis Ababa. Grace Kaneiya na maelezo zaidi. (RIPOTI [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaunga mkono hatua ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu matumzi ya tumbaku

Kusikiliza / Tumbaku

Ikiwa imepita zaidi ya miaka kumi tangu kutekelezwa kwa mkataba wa Jumuiya ya Ulaya kuhusu matumizi ya tumbaku mwaka 2001, Jumuiya ya Ulaya imekuwa kwenye mstari wa mbele katika  kupunguza matumizi ya bidhaa  hizo. Kila mwaka matumizi ya tumbaku na pamoja na madhara ya moshi vimechangia vifo vya zaidi ya watu 700,000 barani ulaya.Kama mwanachama [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Ulaya zingatieni haki za binadamu kwa wahamiaji: wataalamu UM

Kusikiliza / Wahamiaji walionusurika kifo katika mkasa wa Lampedusa , Italia

Mtaalamu wa umoja wa Mataifa kuhusu haki za wahamiaji, François Crépeau, amerejelea tena wito wake kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuangalia upya mtazamo wao kwa wahamiaji na kuhakikisha unazingatia haki za binadamu. Bwana Crépeau akizungumza mjini New York baada ya kukamilika kwa mjadala wa ngazi ya juu kuhusu uhamiaji na maendeleo amesema tukio [...]

07/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wapya ikiwemo Somalia na Bhutan wakaribishwa IPU

Kusikiliza / Nembo ya IPU

Muungano wa mabunge duniani IPU umekaribisha wajumbe wapya ambao ni Bhutan na Somalia katika ufunguzi wa mkutano wake wa 129 mjini Geneva huku Misri ikisubiri kuwa na bunge tena kabla haijajiunga na tena na IPU. Kujiunga kwa Somalia na muungano huo kuliidhinishwa baada ya kuchaguliwa kwa bunge Agost 2012 kama sehemu ya mchakato wa kipindi [...]

07/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban atiwa mashaka na hali inayoendelea CAR

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon atiwa hofu na hali inayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambayo ni ya machafuko, isiyotabirika na isiozingatia sheria. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI) Ban amesema anatiwa woga na ongezeko la mashambulizi ya kulenga na ulipizaji kisasi dhidi ya Waislam na Wakristo [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kazi ya kuharibu silaha za kemikali Syria yaanza

Kusikiliza / Timu ya OPCW ikiondoka kuelekea Syria/picha ya OPCW

Jopo la wataalamu kutoka shirika la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW chini ya usaidizi wa Umoja wa Mataifa limesimamia kazi ya kuharibu silaha za kemikali nchini Syria inayofanywa na watendaji wa nchi hiyo. Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi. (Taarifa ya Alice) Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa watendaji hao walitumia vifaa maalumu kuharibu [...]

07/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »