Nyumbani » 04/10/2013 Entries posted on “Oktoba 4th, 2013”

UM walaani shambulio katika ubalozi wa Urusi nchini Libya.

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja Mataifa wamelaani vikali shambulio lililoelekezwa kwenye ubalozi wa Urusi mjini Tripoli nchini Libya Oktoba mbili mwaka huu na kusababisha uharibifu ikiwamo majengo. Wajumbe wameelezea kusikitishwa kwao kuhusiana na shambulio hilo na kusisitiza umuhimu wa kuwafikisha watekelezaji wa shambulio hilo katika vyombo vya sheria. Pia wamesema matendo kama hayo [...]

04/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ataka wamisri waandamane kwa amani Jumapili

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati wananchi wa Misri wakijiandaa kwa maandamano siku ya Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza umuhimu wa maandamano hayo kufanyika kwa amani bila ghasia yoyote na kuzingatia haki ya watu kukusanyika. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akielezea pia wasiwasi wake kutokana na vurugu kubwa zilizotokea leo [...]

04/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Irina Bokova ateuliwa tena kuwa Mkurugezni Mkuu wa UNESCO

Kusikiliza / Irina Bokova

Bi Irina Bokova ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, ameteuliwa tena kuendelea kuushikilia wadhafa huo kwa muhula wa pili, katika kura ya mchujo ilowajumuisha wagombea wengine wawili. Wagombea hao walikuwa na Bwana Rachad Farah kutoka Djibouti na Joseph Maïla kutoka Lebanon. Uteuzi huo utawasilishwa kwenye mkutano mkuu wa [...]

04/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali ya walimu bado ni dhalili: UNESCO/ILO

Kusikiliza / Mwalimu na mwanafunzi

Tarehe Tano ya mwezi Oktoba kila mwaka ni siku ya walimu duniani. Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake, mathalani lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO na lile la kazi ILO unasema kuwa hali ya walimu bado ni dhalili, wanaishi maisha yasiyo na hadhi, na wakifanya kazi hiyo muhimu katika mazingira duni. Heshima ya walimu [...]

04/10/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Babacar Cissé wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalum Côte d'Ivoire

Kusikiliza / M'Baye Babacar Cissé

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana M'Baye Babacar Cissé wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalum wa Operesheni za Umoja wa Mataifa nchini Côte d'Ivoire, UNOCI, ambako pia atahudumu kama Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa, Mratibu wa Maswala ya Kibinadamu na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP. Bwana Cissé atachukuwa nafasi ya [...]

04/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuwezesha miji kukabiliana na majanga hakuna mjadala: Ban

Kusikiliza / Eneo la makazi likiwa limetwama kwenye maji baada ya mafuriko nchini Pakistani

Katika kuelekea kuadhimisha siku ya makazi duniani, tarehe Saba mwezi huu, shirika la Umoja wa Mataifa la makazi, UN-Habitat limeitisha kikao cha ngazi ya juu kujadili mustakhbali wa makazi hususan mijini ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema mabadilio ya tabianchi yanayoshika kasi, kujenga uwezo wa miji kukabiliana na majanga hakuepukiki. Bwana Ban ametolea mfano wa [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa kimataifa kuzuru maeneo yaliyoathiriwa na ajali ya kinu cha nuklia nchini Japan

Kusikiliza / Nembo ya IAEA

Shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani IAEA litatuma ujumbe wa wataalamu wa kimataifa kwenda nchini Japan baadaye mwezi huu kukadiria shughuli kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ajali ya kinu cha nuklia cha Fukushima Daichi na kutoa habari kuhusu changamoto zilizopo. Kupitia kwa mwaliko wa serikali ya Japan shughuli hiyo itafanyika kati ya tarehe 14 hadi [...]

04/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania iwe makini na uchimbaji wa madini ya Urani: Wataalamu

Kusikiliza / Maeneo ya Uchimbaji Urani

Jopo la wataalamu wa masuala ya nuklia na wale kutoka mtandao wa madini ya Urani, wamesema Tanzania iwe makini katika uchimbaji wa Urani yaliyogunduliwa huko Dodoma na Ruvuma ili kuepuka matatizo yanayoweza kuibuka iwapo hatua stahili hazitachukuliwa. Kutoka dsm, George Njogopa na taarifa zaidi (Taarifa ya George) Wito huu umekuja katika wakati ambapo serikali yaTanzaniainaanzisha [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za kuwasaidia manusura wa ajali ya mashua zaendelea pwani mwa Italia

Kusikiliza / Lampedusa_UNHCR

Jitihada za kuwasaidia manusura kwenye ajali ya mashua pwani mwa kisiwa cha Lampedusa zinaendelea kwa sasa ajali ambayo iligharimu maisha ya raia wa Eritra kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Jason nyakundi na taarifa zaidi. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) UNHCR inasema kuwa idadi ya waliokufa kwenye ajali hiyo ya [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chagizo lahitajika kupiga marufuku hukumu ya kifo kote duniani: IPU

Kusikiliza / Jengo la IPU

Muungano wa Kimataifa wa Wabunge, IPU, umesema ingawa hatua muhimu zimepigwa ama kupiga marufuku hukumu ya kifo au kusitisha utekelezaji wa hukumu hiyo kwa kipindi cha miaka kadhaa, chagizo kubwa zaidi lahitajika kupiga marufuku hukumu hiyo kote duniani. Joshua Mmali na taarifa kamili (Taarifa ya JOSHUA MMALI) Katika kuadhimisha Siku ya Kupinga Hukumu ya Kifo [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi wakimbizi wa kipalestina warejea shule na matumaini

Kusikiliza / Watoto wakikabidhiwa vifaa vya shule

Huko Lebanon hii leo mwaka mpya wa masomo umeanza vyema kwa watoto wakimbizi wa kipalestina wanaoishi nchini humo pamoja na wale waliolazimika kukimbilia Lebanona kutokana na machafukoSyria. Hali hiyo inatokana na msaada wa vifaa vya muhimu vya shule viliyotolewa kwa pamoja na umoja wa Ulaya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Navi Pillay awalilia wahamiaji waliofariki dunia kwenye ajali ya maji Italia

Kusikiliza / Baadhi ya watu walioponea mkasa wa Lampedusa

Mkuu wa Kamishna ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay ameelezea kushtushwa kwake na taarifa za vifo vya wahamiaji wa Afrika waliofariki dunia kwa ajili ya maji wakati wakielekea nchini Italia kwa usafiri wa boti. Pamoja na kuelezea masikitiko yake, Pillay amepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali ya Italia ambayo ilifaulu kuwaokoa baadhi ya [...]

04/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Robo tatu ya watu Mali wakabiliwa na upungufu wa chakula na na mahitaji mengine:WFP/IOM

Kusikiliza / Msaada wa chakula, WFP

Huko Kaskazini mwa Mali, robo tatu ya wakazi wanakabiliwa na hatari ya ukosefu wa chakula. Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 1.3 watahitaji msaada wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014. Tayari shirika la Umoja wa Mataifa la  mpango wa chakula WFP na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM yameanza kufanya tathmini kujua hali halisi ya [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria na Wairaq wanaorejea wanaleta athari kubwa Iraq:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria wakiingia Iraq

Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM iitwayo "Iraq- Athari za mgogoro wa Syria" inasema kwamba kuendelea kuingia kwa wimbi la wakimbizi wa Syria na kurejea nchini kwao kwa wakimbizi wa Iraq waliokuwa Syria kuna athiri nchi nzima lakini hasa jimbo la Iraq la Kurdishan kusababisha kuongezeka kwa changamoto za kijamii, kiuchumi na [...]

04/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ivory Coast yajiunga na mkataba wa kutokuwa na utaifa:UNHCR

Kusikiliza / Ivory coast

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema Ivory Coast imejiunga na mikataba ya kimataifa inayohusu kutokuwa na utaifa. Hii ni moja ya hatua muhimu zinazochukuliwa na serikali hiyo kupunguza idadi ya watu wasio kuwa na utaifa nchini humo. UNHCR inakadiria kuwa watu 700,000 nchini Ivory Coast kwa sasa hawana utaifa au hawana [...]

04/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930