Nyumbani » 02/10/2013 Entries posted on “Oktoba 2nd, 2013”

Ban akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Kusikiliza / Ban Ki-Moon na Waziri Javad Zarif wa Iran

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Javad Zarif. Bwana Ban amekaribisha ujumbe ulotolewa na Iran kwa ujumla katika siku chache zilizopita, na kumpa waziri huyo maelezo kuhusu kutumwa kwa ujumbe wa pamoja ya Umoja wa Mataifa na [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza hatua ya Baraza la Usalama kuhusu usaidizi wa kibinadamu Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha taarifa ya Rais wa Baraza la Usalama iliyotolewa leo na kuridhiwa na wajumbe wa baraza hilo ambayo inalenga kushughulikia hali mbaya ya kibinadamu nchini Syria na kuonyesha azma ya jumuiya ya kimataifa ya kusaidia wananchi wa Syria kuondokana na mzozo unaoendelea kuwakumba. Taarifa ya msemaji wa Umoja [...]

02/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA kuhakikisha ushiriki wa wanawake uchaguziAfghanistan:

Kusikiliza / Wanawake na uchaguzi Afghanistan

Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi za kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao nchiniAfghanistan. Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi maalumu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo Ján Kubiš, mjini Kabul Jumatano. Alikuwa akizungumza na wanawake wanaharakati katika hafla ya kila mwaka inayohusiana na azimio la baraza la usalama [...]

02/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa kupinga uhalifu wa kupangwa waadhimisha miaka 10

Kusikiliza / Maadhimisho ya miaka 10 mkatabawa kupinga uhalifu

Uhalifu wa kimataifa wa kupangwa ni biashara kubwa ambayo faida yake inakadiriwa kuwa dola bilioni 870 kila mwaka, huku ukiathiri idadi isojulikana ya watu. Miaka kumi ilopita, mkakati wa kwanza wa kuupiga vita uhalifu huo ulianza kutekelezwa, kupitia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupinga Uhalifu wa Kimataifa wa Kupangwa, kama hatua ya kujitoa kwa [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kazi ya udhibiti wa silaha za kemikali Syria yaanza rasmi

Kusikiliza / opcw1

Huko Damascus hii leo, jopo linaloendesha operesheni ya kuhakikisha Syria inaondokana na mpango wake wa silaha za kemikali ifikapo katikati mwa mwaka ujao, limekalisha siku ya kwanza ya kazi hiyo. Katika siku hiyo ya kwanza, jopo hilo linalojumuisha wataalamu kutoka shirika la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW na Umoja wa Mataifa limeshirikiana na mamlaka za [...]

02/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laridhia taarifa kuhusu hali ya kibinadamu Syria

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha dharura hii leo limepitisha taarifa ya Rais wa baraza kuhusu hali Mashariki ya Kati hususan nchini Syria ikieleza masikitiko yake juu ya kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na kudorora kwa utoaji wa huduma za msingi za kibinadamu kwa wakimbizi walio ndani na [...]

02/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji sio bidhaa wala chanzo cha matatizo ya kiuchumi na kisiasa: UM

Kusikiliza / migrants boarding ship

Wahamiaji wanatazamwa kama bidhaa au chanzo cha matatizo ya kiuchumi na kisiasa badala ya binadamu, amesema Abdelhamid El Jamri, Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za wahamiaji wafanyakazi. Kamati hiyo imetaka nchi zote kuungana katika mkataba wa kimataifa ambao unalinda haki za kundi hilo ikisema kwa kukubali mkataba huu haina maana nchi [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Sudan Kusini ahaidi kushinda vita dhidi ya HIV:

Kusikiliza / Rais Salva Kiir

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit amesisitiza ahadi yake ya kupanua wigo wa mipango ya kupambana na ukiwmi nchi nzima. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Rais Kiir alipokutana na naibu mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS Luiz Loures mjini Juba amesema Sudan Kusini [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupinga vurugu na ukatili kunahitaji ujasiri: Ban

Kusikiliza / Sananmu ya kupinga ukatili

Leo Oktoba 2 ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Vurugu na Ukatili, na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi, shujaa wa uhuru wa India ambaye aliacha sifa ya kudai haki bila kutumia vurugu. Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuchukua msimamo na kupinga wanaotumia vurugu na ukatili [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malawi na WFP wazindua operesheni kukidhi mahitaji ya chakula:

Kusikiliza / Malawi

Serikali ya Malawi pamoja na shirika la mpango wa chakula duniani na wadau wengine wamezindua operesheni ya misaada ili kukidhi mahitaji ya chakula yanayoongezeka kutokana na hali mbaya ya hewa msimu wa kupanda na kupanda kwa bei Alice kariuki na taarifa kamili: (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Kwa mujibu wa serikali ya Malawi maenmdeo yanayohitaji chakula [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tokomeza ukatili na vurugu dhidi ya watoto: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto huyu alikumbwa na Ukatili

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF katika siku ya kimataifa ya kupinga vurugu na ukatili, limetaka watoto walindwe ili waweze kuishi kwenye mazingira yanayowawezesha kufikia ndoto zao. Taarifa ya UNICEF imesema duniani kote kutwa kucha mamilioni ya watoto wanakumbwa na ghasia iwe shuleni, nyumbani kwenye jamii na mara nyingi vitendo hivyo vinafanyika [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yaandaa mkutano wa kutatua mizozo ya kikabila jimbo la Darfur

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

Zaidi ya viongozi 100 wa makabila kwenye jimbo la Darfur kutoka makabila yote kaskazini mwa Darfur walikusanyika kwenye mkutano wa siku mbili kujadili janzo cha ghasia za kikabila kwenye jimbo la Darfur ambapo walipendekeza suluhu ya kuleta amani katika eneo hilo. Mkutano huo ulioandaliwa na ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa [...]

02/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

HAI yawasaidia wakimbizi Kipalestina waliokuwa Syria na sasa wamehamia Jordan

Kusikiliza / Wakimbizi wa Kipalestina

Mashirika mawili ya ustawi wa binadamu,lile la Human Appeal International lenye makao yake huko Emirate, Ajman na lile linalozingatia hali bora kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA yamekubaliana kuwapa msaada wakimbizi wa Kipalestina waliokokuwa wakiishi nchini Syria ambao sasa wamekimbilia nchi jirani ya Jordan. Masharika hayo yamekubaliana kwa pamoja kuwaangazia wakimbizi hao kwa kuwasambazia huduma muhimu [...]

02/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa Kenya Walter Barasa

Kusikiliza / Icc

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa Kenya, Walter Osapiri Barasa kwa madai kadhaa ikiwemo kuingilia mwenendo kwa kesi zinazowakabili raia waKenyaambazo zinaendelea kwenye mahakama hiyo. Hati hiyo iliyotolewa leo inazingatia maelezo ya msingi yaliyotolewa na upande wa mashtaka ambapo Jaji Cuno Tarfusser amesema yanatosheleza kumkamata mwandishi [...]

02/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasema imezidiwa nguvu na ongezeko kubwa la wakimbizi

Kusikiliza / Mkutano wa UNHCR Geneva

Kamishna wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR António Guterres amesema kuwa mamia ya watu wameendelea kukimbia makazi yao jambo ambalo linazidisha hali ya wasiwasi kwani idadi ya wakimbizi wanajitokeza sasa hajapata kushuhudiwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Kamishna huyo ameiambia Kamati ya Utendaji inayokutana kwa mkutano wake wa kila mwaka kuwa,ongezeko [...]

02/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Meno ya ndovu, ugaidi ni vita ya kiamataifa :Kikwete

Kusikiliza / MSAMI NA KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amesema ujangili wa pembe za ndovu na faru ni tatizo la kimataifa linaolohitaji kutokomezwa kwa ushirikiano huku akitaka mataifa makubwa kudhibiti soko la pembe hizo ,hatua ambayo amesema inaweza kukomesha uwindaji haramu unaoathiri utalii barani Afrika. Katika mahojiano amaaluma na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa [...]

02/10/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930