Nyumbani » 01/10/2013 Entries posted on “Oktoba 1st, 2013”

Mkutano juu ya mkataba wa Minamata kufanyika Japan

Kusikiliza / unep

Pande zinazohusika na mkutano wa kimataifa ujulikanao kama " mkataba wa Minamata juu ya madini ya Zebaki" unatazamiwa kufanyika huko Minamata na Kumamoto nchini Japan kuanzia Octoba 9 hadi 11 mwaka huu. Madini ya Zebaki ni moja ya zingatio kubwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na kile kianchosemwa kwamba kemikali zake huzusha kitosho cha dunia [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kifo cha askari wa Sierra Leonne huko Sudan

Kusikiliza / UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amesikitishwa na kifo cha askari mshauri kutoka Sierra Leone ambaye alijeruhiwa katika shambulio dhidi ya askari walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani Darfur , UNAMID, July 13 ambapo askari saba walinda amani kutoka Tanzania waliuwawa. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini New [...]

01/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tuangalie maneno na vitendo vya Iran: Netanyahu

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Pazia la Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefungwa rasmi Jumanne mchana kwa hotuba kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ambayo kwa kiasi kikubwa ililenga masuala ya nyuklia ikigusiaIran. Bwana Netanyahu katika hotuba yake amesema anashindwa kujiaminisha kwa dhati kwa kauli za Rais wa Iran Hassan Rouhani alizotoa hivi karibuni [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasikitishwa na mauaji ya watoto 12 Syria

Kusikiliza / unicef-logo

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesikitishwa na kuripotiwa kwa vifo vya watoto 12 katika shambulizi la angani dhidi ya shule moja ya sekondari eneo la Ragga, kaskazini mashariki mwa Syria, mnamo tarehe 29 Septemba. Ripoti kutoka eneo la tukio zinasema watu 14 – wengi wao wanafunzi- waliuawa katika shambulizi hilo dhidi [...]

01/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Timu ya OPCW na ya UM yawasili Damascus na kuweka kituo:

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na ya kupinga matumizi ya silaha za kemikali OPCW, imewasili nchini humo siku nne baada ya baraza la utendaji la OPCW na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha bila kupingwa mipango ya kutuma timu hiyo Syria kuanza mchakato wa kusimamia kazi ya kuharibu mipango ya silaha [...]

01/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yajadili afya za wasafiri mipakani na nchi za Kusini mwa Afrika

Kusikiliza / iom logo

Nchini Tanzania, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM leo limehitimisha mkutano wake wa siku uliowakutanisha wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kujadilia mkakati wa pamoja wa afya kwa wasafiri maeneo ya mipakani pamoja na madereva wa magari makubwa ambao wanakabiliwa na hatari ya kukubwa na magonjwa ya kuambukizwa. Kutoka dsm, George Njogopa na taarifa [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano mkuu kujadili agenda ya maendeleo ya wahamiaji:IOM

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

Mjadala mkuu kuhusu uhamiaji wa kimataifa na mendeleo unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mjiniNew York ambapo mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yatajumuishwa katika kupanga sera na mikakati ya kundihilokatika mkutano unaoanza jumatano.  Msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, Jumbe Omari Jumbe katika mahijiano na idhaa hii anasema shirika hilo lina agenda muhimu [...]

01/10/2013 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Ban na Waziri Amina wazungumzia Somalia, ICC na wakimbizi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Bi. Amina Mohammed mjiniNew York, ambapo kwa mara nyingine tena Ban ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi kufuatia shambulio la mwezi uliopita huko Nairobi. Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa usaidizi kwa kadri [...]

01/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Syria na mataifa jirani yatia wasi wasi

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

  Shrika la mpango wa chakula duniani WFP limeelezea wasi wasi uliopo kutokana na hali ilivyo nchiniSyriana mataifa jirani kutokana kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohama makwao walioathiriwa na kuzorota kwa  uchumi . Watu waliohama makwao hawana uwezo wa kununua kutokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa. Mavuno duni mwaka huu . Ikiwa inawafikia watu [...]

01/10/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utesaji magerezani wazidi kuongezeka Libya

Kusikiliza / Ravina Shamdasani

Ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu inasema  kuwa vituo vingi vya magereza  nchini Libyabado vinaendelea na mwenendo wa kutesa watu na kuwapa huduma zisizostahili. Alice Kariuki na taarifa kamili (TAARIFA YA ALICE ) Ripoti hiyo imesema kuwa vitendo hivyo vya utesaji mara nyingi hufanyika wakati watuhuiwa wanapotiwa nguvuni [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNCEF yatoa msaada kwa zaidi ya familia 5000 kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati

Kusikiliza / Wakimbizi CAR

  Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linatoa misaada ya dharura kwa zaidi ya watu 5,500 ambao wamelazimika kuhama makwao kwenye maaeno yaliyo kaskazini mwa Jamahuri ya Afrika ya Kati. Asilimia kubwa ya wale waliohama makwao ni  wanawake na watoto ambao sasa wanaishi katika mazingira mabaya wakiwa hawana maji wala makao. Karibu [...]

01/10/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa dharura Geneva waafikia kuongeza usaidizi kwa nchi zinazohifadhi wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko kambi ya Za'atri, Jordan

Jamii ya kimataifa imeafikia kuchukua hatua za dharura ili kuzisaidia nchi jirani za Syria, ambazo zinaubeba mzigo wa kijamii na kiuchumi kwa kuwapa hifadhi zaidi ya wakimbizi milioni mbili wa Syria, huku Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP likielezea wasiwasi wake kutokana na kusambaratika kwa uchumi na tatizo la chakula nchini humo. Joshua Mmali [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugaidi usipodhibitiwa utaathiri ajenda ya maendeleo: Botswana

Kusikiliza / Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana, Phandu Skelemani

Hatimaye mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefikia ukingoni hii leo kwa watoa hotuba kuzungumzia amani, ulinzi, usalama, mazingira na maendeleo duniani. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Siku ya mwisho ya mjadala mkuu, wajumbe walipokea ripoti kutoka kwa wawakilishi wa nchi na maeneo kama vileMaldives,Botswanana Holy See. Mathalani Waziri [...]

01/10/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mpango wa kwanza wa kutokomeza vifo vya TB kwa watoto waainishwa:WHO

Kusikiliza / Children Kenya

Mpango wa kwanza unaoainisha hatua za kuchukuliwa kutokomeza vifo vitokanavyo na kifua kikuu umezinduliwa Jumanne nchini Marekani limesema shirika la afya duniani WHO. Flora Nducha na taarifa kamili (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Vifo zaidi ya 74,000 vya watoto vitokanavyo na kifua kikuu vinaweza kuzuilika kila mwaka kupitia hatua zilizoainishwa katika mpango huo wa kwanza maalumu [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wazee wana haki ya kuishi maisha yenye staha: Ban

Kusikiliza / Older people Mozambique

Katika kuadhimisha siku ya wazee duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametaka serikali kujizatiti kuondoa vikwazo vyote vinavyowanyima wazee haki zao za msingi na kuwafanya waishi maisha yasiyo na staha. Ujumbe wa Bwana Ban unaeleza bayana kuwa idadi kubwa ya wazee wanaishi maisha dhalili katika jamii zao wakihaha kupata huduma [...]

01/10/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031