Viongozi Afrika wakerwa na ICC kumulika viongozi wa Afrika pekee

Kusikiliza /

ICC-building3

Suala la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC kuwagusa  viongozi wa Afrika pekee limeibuka wakati wa mkutano baina ya wawakilishi wa nchi za Afrika Mashariki na shirika la kimataifa la maendeleo IGAD ambapo mjadala wa kina kuhusu swala hilo utafanyika Ijumaa wiki hii. Grace Kaneiya anaarifu

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe amesema viongozi wa Afrika wameonyeshwa kukerwa na suala hilo na hivyo watawakilisha mawazo yao katika mjadala huku akisema hata mfumo wa uendeshaji kesi wa ICC hautoi fursa kwa viongozi watuhumiwa kuendelea na kazi zao mathalani kwa kesi inayomuhusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na Makamu wake William Ruto.

(Sauti Membe)

Naye Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na Idhaa hii ameunga mkono maoani hayo

(CLIP YA MUSEVENI)

Mjadala huu unakuja siku chache baada yaKenyakupiga kura ya kutaka kujiondoa kuwa mwanachama wa ICC.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031