Vimbunga vyasababisha maafa Mexico: Ban atuma rambirambi

Kusikiliza /

Mwananchi wa Mexico akijitahidi kukabiliana na mafuriko yatokanayo na kimbunga Manuel

Wakati maafa yaliyotokana na vimbunga Manuel na Ingrid yakiendelea kuwa dhahiri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kushtushwa kwake na vifo vya watu kutokana na janga hilo pamoja na uharibifu wa mali na makazi. Vimbunga hivyo vilivyoanza tarehe 17 mwezi huu vimeathiri watu zaidi ya Milioni Moja huku hali ya tahadhari ikiwa imetangazwa kwenye manispaa kadhaa zilizo Ghuba ya Mexicona pwani ya Pasifiki na mvua zaidi zikiendelea kutarajiwa. Katibu Mkuu ametuma rambi rambi kwa serikali yaMexicona wananchi wake hususan familia zilizopoteza jamaa huku akielezea mshikamano wa dhati na wahanga wa janga hilo. Bwana Ban amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa usaidizi wowote kwa mahitaji yatakayojitokeza kutokana na vimbunga hivyo pamoja na kusaka misaada ya kimataifa inayohitajika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031