Vijana wataka uwazi zaidi katika uongozi

Kusikiliza /

Mkutano wa vijana wang’oa nanga, Costa Rica

Vijana kutoka kila pembe ya dunia wametoa wito kwa viongozi wa wa dunia kutoa njia rahisi zaidi, za nguvu, na za wazi za masuala ya uongozi ambazo zitawafikia watu wengi zaidi kuliko za sasa.

Wito huo umekuja katika azimio la vijana lililopatikana kwenye mkutano wa siku tatu wa maendeleo na teknolojia ya mawasiliano baada ya mwaka 2015 uliofanyika wiki hii nchini Costa Rica.

Waraka wa wito wao umekabidhiwa Alhamisi kwa Rais wa nchi hiyo Laura Chinchilla, ambaye atauwasilisha kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa litakapoanza mjadala wake baadaye mwaka huu.

Azimio la vijana hao linasisitiza kwamba ubunifu utakuwa muhimu kwa maendeleo na mfumo wa elimu ambao utawapa wanafunzi nyezo na ujuzi ambao unahitajika katika uchumi wa dunia ya kidigital.

Mkutano huo wa mtazamo wa baada ya 2015 umeandaliwa na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU na umeshirikisha vijana zaidi ya 600 walioshiriki moja kwa moja na wengine 4000 walijiunga na mjadala.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930