UNHCR yasifu kusudio la Bulgaria la kuleta matumaini kwa waomba hifadhi

Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya serikali ya Bulgaria ya kuahidi kuboresha mazingira ili kuwawezesha raia wa Syria na wengine wanaoomba hifadhi kuishi katika hali bora, katika wakati ambapo nchini hiyo ikabiliwa na ongezeko la wahamiaji. Alice Kariuki na maelezo zaidi:

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Katika utekelezaji wa suala hilo, tayari Mwakilishi wa UNHCR kwa nchi za Ulaya ya Kati Montserrat Feixas Vihe, amekutana na Waziri Mkuu Plamen Oresharski ambao wote pamoja wamejadiliana juu ya umuhimu wa kutolewa kwa vifaa vipya kwa ajili ya kuwawezesha wahamiaji hao kuishi katika mazingira mazuri.

Pia wamezungumzia uwezekano wa kuwaachia huru baadhi ya wahamiaji waliotiwa korokoroni hatua ambayo italeta ahueni kutokana na msongamano mkubwa unaojitokeza kwenye maeneo wanayoshikiliwa.

Katika kipindi cha mwaka huu pekee, Bulgaria imepokea maombi 3,000 kutoka kwa watu wanaoomba hifadhi wengi wao wakitoka Afrika na Mashariki ya Kati. Kiwango hicho kinatajwa kuwa kikubwa zaidi ya mara tatu ililinganishwa na maombi mengine ya muongo mmoja uliopita. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031