UNHCR yakaribisha uamuzi wa Brazil kutoa viza kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

Wahamiaji wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya kamati ya kitaifa ya Brazil iliyoeleza kusudia lake la kutoa vibali vya kuingia nchini humo au viza kwa raia wa Syria na wan chi nyingine ambao wameathirika na mapigano yanayoendelea.

 Kamati hiyo CONARE imesema kuwa iko tayari pia kutoa viza kwa wale wanakusudia kuomba ukimbizi nchini Brazil. George Njogopa na taarifa kamili.

 

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ofisi za ubalozi  wa Brazil zilizoko katika nchi jirani na Syria ndizo zitakazowajibika kutoa viza hizo na kwamba hati za ukimbizi zitatolewa wakati watapowasili.

Kuna idadi ndogo ya wakimbizi wa Syria wanakwenda nchini Brazil na hadi sasa kamati ya CONARE imewatambua waomba hifadhi 280.

UNHCR imeyatolea mwito mataifa kutoa msaada kwa wakimbizi 10,000 ambao wanahitaji hifadhi katika mataifa ya nje ndani ya mwaka huu 2013. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031