UNEP yakaribisha maelewano mapya ya kuondoa gesi zinazochafua mazingira

Kusikiliza /

Gesi zinazoharibu tabaka la ozone

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limekaribisha maafikiano kutoka kwa viongozi wa dunia kwenye mkutano wa mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi ya G20 mjini Moscow ya kutumika kwa mbinu mpya katika kupunguza gesi zinazochafua mazingira zinazojulikana kama hydrofluorocarbons. Alice Kariuki na taarifa kamili

 (TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Serikali kutoka nchi 25 na Jumuiya ya Ulaya wamekubaliana kwamba kuondoa matumizi ya gesi za hydrofluorocarbons yaliyofanywa sambamba na kupunguzwa kwa gesi ya Carbon Dioxide chini ya mpango ulio kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa unaohusika na mabadiliko ya hali ya hewa kutatoa mchango mkubwa kukabiliana na adhari za mabadiliko ya hali hewa. Gesi hizo zinatumika kwa wingi viwandani zikichukua nafasi ya zile zinazoharibu tabaka la Ozoni zinazoondolewa kupitikia kwa makubaliano ya Montreal.

Kuwepo kwa gesi za hydrofluorocarbons ni chini ya asilimia moja lakini athari zao kwa viwango vya joto duniani  ni za juu kuliko gesi ya Carbon. Kulingana na Shirika UNEP ni kwamba hatua za mapema dhidi ya gesi za hydrofluorocarbons kutapunguza  kuongezeka kwa joto duniani kwa nyusi 0.5 , kuzuia kupotea kwa tani milioni 30 kila mwaka na kuokoa maisha kwa kupunguza magonjwa wa kupumua.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031