UN-WOMEN yalaani mauaji ya maafisa wa serikali wa kike Afghanistan

Kusikiliza /

Phumzile-Mlambo-Ngcuka, Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women

Kitengo cha masuala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women, kimelaani vitisho na mauaji yanayowalenga wanawake ambao ni maafisa wa serikali, na kutoa wito hatua za kisheria zichukuliwe. Assumpta Massoi na taarifa kamili

(Taarifa ya Assumpta)

Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women Phumzile Mlambo-Ngcuka imesema visa vya hivi karibuni vya mauaji yanayolenga wanawake wenye nyadhifa serikalini,  vinatoa hitajio la dharura la kuhakikisha serikali ya Afghanistan inaweka mazingira ya haki kwa kundi hilo pamoja na watoto wa kike wakati huu ambapo serikali inaandaa kushika hatamu za ulinzi kutoka kwa vikosi vya kimataifa, na kufanya uchaguzi wa majimbo na wabunge. Mkuu huyo wa UN-Women amesema uwezeshaji wanawake na kuhakikisha wanapata haki zao ni msingi mkuu wa ujenzi wa Afghanistan ili wanawake na wanaume waweze kuwajibika kwa mustakkbali wa maendeleo ya nchi yao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031