UM yatilia shaka kutoroka gerezani kwa askari

Kusikiliza /

Martin Kobler

Afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ameeleza kushtushwa kwake kutokana na taarifa za kutoroka gerezani kwa askari wawili wa Congo  ambao walitiwa hatiana kutonana na mauwaji yaliyoyatenda.

Askari hao ambao hadi sasa hawajulikani walikotokomea pia walikutikana na hatia ya kushiriki vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo ubakaji na mauwaji ya mamia ya raia.

Katika taarifa yake kufuatia tukio hilo Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler ameitaka serikali kuchukua ulinzi wa kutosha kwa mashahidi pamoja na wanasheria waliosimamia kesi hiyo.

Askari hao waliokuwa katika gereza Bukavu Mashariki mwa jimbo la Kivu Kusin wanaarifiwa kutoroka Septemba 21 na 22 ikiwa ni muda wa wiki mbili tangu walipohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930