Ulimwengu una uwezo na jukumu la kuumaliza mzozo wa Syria: UM

Oscar Fernandez-Taranco, Msaidizi wa Katibu Mkuu kwa masuala ya kisiasa

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zina uwezo na jukumu la kukabiliana na mzozo wa Syria, ambao umetajwa na kuwa changamoto kubwa zaidi kwa amani na usalama ulimwenguni, na kukomesha ukatili ambao raia wa Syria wanaendelea kupitia.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, katika taarifa ilotolewa na msaidizi wake wa masuala ya kisiasa, Oscar Fernandez-Taranco, wakati wa mkutano wa mawaziri wa nchi marafiki za watu wa Syria.

Hakuna suluhu la kijeshi kwa mzozo wa kisiasa nchini Syria. Njia pekee ya kuleta amani nchini humo na kwa watu wake, ni kupitia kwa mazungumzo na kulegeza misimamo ya kisiasa. Kongamano la Geneva kuhusu Syria, ambalo Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila uwezalo kuandaa kwa miezi kadhaa, linalenga kuzindua mazungumzo kama hayo.”

 Kulingana na taarifa hiyo, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon anaamini kuwa kongamano la Geneva litafanyika hivi karibuni, na kwamba litafanikiwa kulimaliza janga lililopo Syria.

Amesema anatumai mkutano wa leo utatoa jukwaa la uungwaji mkono mkubwa wa kisiasa kwa ushiriki wa muungano wa kitaifa wa upinzani nchini Syria katika kongamano la Geneva.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29