Ukanda wa Sahel bado kuna changamoto, tushirikiane kusaidia: Ban

Kusikiliza /

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu ukanda wa Sahel na kusema kuwa mwaka mmoja baada ya mjadala kuhusu eneo hilo, juhudi za pamoja zimesaidia kuimarisha hali ya usalama, kisiasa na hata kuna mikakati ya kushughulikia changamoto kubwa. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi:

(Taarifa ya Alice)

Kikao hicho kimefanyika kando mwa mjadala wa Baraza Kuu ambapo Bwana Ban amesema hali bado si nzuri sana kiafya, kijamii, kiuchumi na kiusalama ambapo biashara ya dawa za kulevya inatishia eneo hilo, vikundi vyenye silaha hali kadhalika, na watu Milioni Moja hawana uhakika wa chakula. Amesema changamoto hizo zimetangamana lakini ni vyema kuchukua hatua za pamoja kitaifa, kimataifa na kikanda kusaidia wakazi wa Sahel. Amesema mkakati ulioandaliwa chini ya uongozi wa mjumbe wake maalum kwenye eneo hilo Romano Prodi unatoa kipaumbele kwa utawala bora, usalama na kuwezesha watu kukabiliana na matatizo. Hata hivyo amesema …

(Sauti ya Ban)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29