Ujerumani yawapatia wasyria Elfu Tano makazi ya muda: IOM

Kusikiliza /

Serikali ya Ujerumani imekubali kuwapatia ukazi wa muda raia elfu Tano wa Syria wanaoishi Lebanon, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM.

Wakimbizi hao wametambuliwa na UNHCR na watasafirishwa kwa ndege maalum zilizokodishwa na IOM kutoka Beirut kwenda Hanover Ujerumani katika kipindi cha mwaka mmoja.

Tayari IOM imeaanza kutoa mafunzo ya makazi mapya ikiwemo ya utamaduni, lugha kwa wakimbizi 109 kati yao ambao wataondoka katikati mwa mwezi huu. Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anasema wakimbizi hao watakuwepo Ujerumani kwa kipindi hadi itakapokuwa salama kwao kurejea nyumbani na kuishi maisha ya staha.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Lebanon inaendeza sera yake ya kuacha mpaka wazi na kwa sasa ina wakimbizi zaidi ya Laki Saba kutoka Syria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031