Uchaguzi ujao Sri Lanka ni muhimu kwa maridhiano ya kisaiasa:Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameukaribisha uchaguzi ujao wa mikoani nchini Sri Lanka mnamo Septemba 21, hususan katika Mkoa wa Kaskazini ambako huu utakuwa uchaguzi wa kwanza tangu mabaraza ya mikoa yalipoundwa mnamo mwaka 1987.

Katika taarifa iliotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema anauona uchaguzi huo kama nafasi muhimu ya kuleta maridhiano ya kisiasa na kujenga imani miongoni mwa raia wa Sri Lanka baada ya miaka mingi ya migogoro.

Ametoa wito kwa wahusika wote kushiriki uchaguzi huo kwa amani na kufanya kazi pamoja baada ya uchaguzi ili kukabiliana ajenda ya kitaifa baada ya vita, kwa njia ya kujenga na ushirikiano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031