Tisho la ugaidi sasa ni dhahiri, mafunzo maalum yatolewa:Kikwete

Kusikiliza /

Rais Jakaya Kikwete akihojiwa na Joseph Msami wa Radio ya UM

Rais wa Tanzanaia Jakaya Kikwete amesema ni dhahiri kwamba tishio la ugaidi ni sehemu ya maisha ya sasa na kwamba nchi yake iko katika hali ya tahadhari na ili kujihami vyombo vya usalama vimepewa mafunzo maalum.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya Radio y a Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema mara kadhaa idara ya usalama imekuwa ikipokea taarifa ya uwezekano wa mashambulizi na hivyo kuchukua hatua.

 (SAUTI YA KIKWETE)

Rais huyo wa Tanzania alisaini kitabu cha maombolezo kwenye ubalozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa mjini New York akitoa pole kwa nchi hiyo kufuatia vifo zaidi ya 60 na majeruhi zaidi ya mia moja baada ya magaidi kushambulia eneo la maduka makubwa, Westgate jijini Nairobi hivi karibuni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31