Sera za taifa kuhusu uhamiaji zijali wananchi: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Wakati idadi ya watu wanaoishi uhamishoni ikifikia zaidi ya milioni 215, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Navi Pillay amezikumbusha serikali duniani kote kutambua kwamba uhamiaji ni nguzo muhimu kwa watu na ametaka kuundwa kwa sera zitakazosaidia kutatua kasoro zinazokwamisha haki za binadamu. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

 (Ripoti ya Alice)

Akizungumza na jopo la wataalamu wa uhamiaji, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa uhamiaji ni nguvu muhimu inayogusa maisha ya watu ambao wanasafiri huku na kule kwa ajili ya kusaka fursa za uchumi na kisiasa.

Amesema kuwa hivi sasa suala la watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi jingine ni suala lisiloepukika hivyo amehimiza haja ya kuandaliwa sera zitazochochea ufanisi wa idara za uhamiaji. Kauli ya Pillay imekuja katika wakati ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likijiandaa,kukutana mwezi ujao kujadiliana juu ya uhamiaji. Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika Oktoba 3 utawahusisha viongozi wa ngazi za juu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29