Rwanda yaongoza kuwa wabunge wengi wanawake duniani:IPU

Kusikiliza /

Jengo la IPU

Muungano wa mabunge duniani IPU unasema wabunge wanawake nchini Rwanda hivi sasa ni karibu theluthi mbili ya wabunge wote kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki hii.

IPU inasema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Rwanda takribani asilimia 64 ya viti vyote vya bunge la chini vinashikiliwa na wanawake ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka asilimia 56.3 ya bunge lililopita.

Na kwa mantiki hiyoRwandainaendelea kuwa ndio bunge pekee duniani ambalo wabunge wanawake ndio idadi kubwa zaidi na kuifanya Rwanda kushikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa na wabunge wengi wanawake duniani.

Rwandaimekuwa ikiongoza tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 ingawa asilimia 30 ya viti vya bunge imetengwa maalumu kwa ajili ya wanawake nchi hiyo imeshapita asilimia hiyo katika chaguzi mbili zilizopita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031