Rais Kabila ajadili na Ban hali ya Dr Congo

Kusikiliza /

Katibu Mkuu, Ban Ki-moon na rais wa DR Congo Joseph Kabila Kabange

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange leo amekuwa na mkutano na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kando ya mjadala wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Katika mkutano wao wamebadilishana mawazo kuhusu hali ya Dr Congo na ukanda wote wa maziwa makuu ikiwemo hatua ya mazungumzo ya Kampala.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu haja ya pande zote zilizotia saini mkataba kutekeleza mpango wa amani , usalama na ushirikiano. Katibu Mkuu ameichagiza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuendelea na juhudi zake kutekeleza ahadi zake za kitaifa na kuendelea kuonyesha uongozi shupavu katika kukabiliana na ukatili wa ngono.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930