OCHA yaelezea hofu yake dhidi ya mauaji ya raia Ituri

Kusikiliza /

Nembo ya OCHA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limeelezea hofu yake juu ya mauaji ya raia 10 wakiwemo wafanyakazi watatu wa afya kwenye eneo la Geti wilaya ya Ituri jimbo la Orientale nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

OCHA inasema mauaji ya raia na mauaji ya aina yoyote ile nchini humo hayakubaliki na hayawezi kuahalalishwa kwa sababu yoyote ile. Yens Laerke ni msemaji wa shirika la OCHA.

Mapigano baina ya vikosi vya serikali na kundi la Ituri la FRP yalishika kasi mapema mwezi huu na watu 60,000 kulazimika kuzikimbia nyumba zao katika maeneo ya Irumu Kusini Ituri, na watu zaidi ya 100,000 hivi sasa wanahitaji msaada wa haraka.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930