Mtalamu huru wa UM asifu mwelekeo wa haki za binadamu Somalia

Kusikiliza /

Shamshul Bari

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia Shamsul Bari amepongeza kupitishwa kwa mpango wa utekelezaji na usimamizi wa haki za binadamu nchini humo. Bari amesema kitendo hicho cha serikali ya Somali kinaweka msingi wa kuimarisha uendelezaji na ulinzi wa haki za binadamu. haki za binadamu.

Hata hivyo ametaka serikali kupanua wigo wa mchakato wa mashauriano ili kujumuisha zaidi serikali za mikoa na vikundi vya kiraia. Mpango huo ulipitishwa rasmi tarehe 27 mwezi ujao katika kikao maalum cha baraza la mawaziri kilichoitishwa na Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon ambapo katika kikao hicho ilitangazwa rasmi kuwa tarehe 27 Agosti ya kila mwaka ni siku ya kitaifa ya haki za binadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930