Monique Barbut ateuliwa kuwa katibu mkuu wa UNCCD

Kusikiliza /

Monique Barbut

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kufuatia majadiliano na ofisi ya Umoja wa mataifa inayohusika na mkataba wa kukabiliana na hali ya jangwa UNCCD leo ametangaza uteuzi wa Monique Barbut wa Ufaransa kuwa katibu mkuu wa UNCCD.

Bi. Barbut anachukua nafasi ya Bwana Luc Gnacadja. Ban amemshukuru bwana Gnacadja kwa mchango na kazi kubwa aliyoifanya kutekeleza kazi za Umoja wa Mataifa. Bi Barbut atachukua wadhifa huo na kuja na uzoefu mkubwa alionao katika masuala ya kimataifa ya diplomasia na siasa

Bi Barbut ameshika nyadhifa mbalimbali 2012 amekuwa mshauri wa mkuu wa shirika la Ufaransa la maendeleo na kabla ya hapo alikuwa mkuu na mwenyekiti wa Global envriroment facility kuanzia 2006 hadi 2012.

Nyadhifa zingine alizowahi kuhudumu ni kama mkurugenzi wa idara ya teknolojia , viwanda na uchumi ya shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP 2003 hadi 2006.

Bi. Barbut ana shahada ya udhamili katika masuala ya uchumi na shahada ya kwanza ya lugha ya Kiingereza alizozipata katika chuo kikuu cha Paris. Alizaliwa mwaka 1956 nchini Morocco, ameolewa na ana watoto watatu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29