Mkuu wa UNESCO alaani shambulio kwenye msikiti wa kihistoria Timbuktu

Kusikiliza /

Irina Bokova

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Irina Bokova ameshutumu vikali shambulio la kujilipua karibu na msikiti wa kihistoria wa Djingareyber huko Timbuktu nchini Mali. Taarifa ya UNESCO imemkariri Bi. Bokova akituma rambirambi kwa wafiwa na majeruhi huku akisema shirika lake limejizatiti kuhifadhi mali za kihistoria ikiwemo msikiti huo wa Djingareyber ulio katika orodha ya urithi wa dunia. Tayari msikiti huo ulikumbwa na zahma wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali na wasi wa Tuareg mapema mwaka jana. Msikiti huo ambao pia unajumuisha Chuo Kikuu cha Timbuktu yaaminika ulijengwa mwaka 1327 kwa kutumia miti mabua na miti mibichi ikipatiwa uthabiti na chokaa. Mapema mwaka huu wataalamu wa Umoja wa Mataifa waliridhia mpango wa kukarabati na kulinda urithi wa kitamaduni wa Mali kwa gharam ya dola Milioni 11.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031