Mkuu wa MONUSCO alaani vikali mashambulizi dhidi ya shule na hospitali:

Kusikiliza /

 

Martin Kobler

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umelaani vikali mashambulio dhidi ya shule na hospitali yanayofanywa na pande zinazoshirikia vita na hususani kundi la watu wenye silaha la ADF katika eneo la Beni.

Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler amesema ADF na pandezote zinazoshiriki vitendo hivyo ni lazima waache mara moja kwani ni vitendo vinavyokiuka haki za mtoto. Amesema vitendo hivyo vimewanyima fursa watoto zaidi ya 7000 kupata elimu na athiri mfumo wa huduma za afya kwa maelfu yaw engine.

Kufuatia uchunguzi wa pamoja wa MONUSCO na uongozi wa eneo la

Kamango himaya ya Beni, imebainika kwamba ADF walivamia shule 11 za msingi na vituo vitano vya afya mwezi Julai mwaka huu na kuharibu samani za shule, kuiba madawa na vifaa vingine vya kitabibu. Kuanzia Novemba 2012 na Mai 2013 ADF imeshambulia vituo vingine vine zaidi vya afya na shule pia katika mji wa Beni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29