Mkutano wa idadi ya watu Asia-Pacific kuzingatia maisha bora

Kusikiliza /

Mkutano wa 6 walenga maisha bora

Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa sita wa idadi ya watu kwa Asia na Pacific wanatathimini idadi ya watu na changamoto za maendeleo zinazokabili kanda hiyo ikiwemo ongezeko la kasi la wazee, wahamiaji na mfumo wa familia.

Mkutano huo unaojumuisha wajumbe kutoka nchi zote za Asia na Pacific utajadili masuala mengine yanayotoa changamoto na ambayo ni muhimu sana kama haki za binadamu na maendeleo, ikiwemo pia afya ya uzazi na haki zake, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, HIV na ukimwi, ukatili wa kijinsia na haki za vijana.

Kwa mujibu wa mkutano huo katika kanda ya Asia na Pacific wanawake wengi bado wanakufa kutokana na kujifungua. Mkutano huo wa siku tano ulioanza Jumatatu unatarajiwa kutoka na suluhu za kushughulikia changamoto za idadi ya watu na maendeleo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031