Mkutano wa IAEA waangazia sayansi ya aisotopiki na nyuklia katika ulinzi wa mabahari

Kusikiliza /

                                                                                                     Wanasayansi wa uhai wa majini kutoka kote duniani wanakutana mjini Vienna, Austria kuanzia leo ili kujadili tatizo la kuongezeka kwa viwango vya asidi katika mabahari, hatari zake, na jinsi ya kukabiliana nalo. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, bayo anuai ya majini inayolinda usalama wa mabahari inaendelea kupata shinikizo kubwa, kwani viwango vya asidi vinaongezeka kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa. Hali hii inatia uhai wa viumbe wa majini hatarini, na wote wanaotegemea mabahari. Sayansi inayotumia mbinu za aisotopiki, ambayo huratibiwa na IAEA, husaidia sana katika kuelewa jinsi asidi inavyoongezeka katika mabahari na athari zake. Akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Yukiya Amano, amesema katika kukabiliana na vitu vinavyotishia ubora wa mabahari, serikali zinahitaji takwimu zilizo sahihi. Hivyo basi, amesema watafiti wenye ustadi mkubwa wanahitajika ili wabuni njia mwafaka za kubashiri hali ya baadaye, ili serikali zianze kutekeleza mbinu bora za kulinda mabahari.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31