Mke wa Rais wa Uganda aongeza juhudi za ahadi ya vita dhidi ya ukimwi:

Kusikiliza /

Bi Janet Museveni

Mke wa Rais wa Uganda Bi Janet K Museveni, amedhihirisha juhudi zake za kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya HIV kwa watoto kwa kupeleka kampeni ya kitaifa katika eneo la Karamoja, moja ya mikoa isiyojiweza katika nchi hiyo.

Bi Musevern amezindua kampeni ya "kutokomeza maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa motto" Septemba 16 mwaka huu katika mji wa Moroto.

Kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuzuia maambukizi ya HIV miongoni mwa watoto kwa kuchagiza matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya HIV kwa kina mama wajawazito ambao wanaishi na virusi. Kampeni hiyo inakwenda sambamba na utekelezaji wa maagizo ya shirika la afya duniani WHO .

Mkurugenzi wa UNAIDS Michele Sidibe akisifu juhudi hizo amesema ukimwi unaweza kudhibitiwa na Afrika inaweza kupata matibabu, kwani juhudi zinafanyika kwa ujasiri, uongozi imara na ushirikiano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930