Mjumbe wa UM nchini Somalia anasema kuwa usalama ndiyo changamoto kubwa zaidi nchini Somalia

Kusikiliza /

Nicholas Kay

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay ametoa wito wa kutaka kutolewa kwa msaada ya kifedha na ya kijeshi kusaidia jitihada za muungano wa Afrika katika keleta amani na usalama nchiniSomalia. Taarifa ya Jason Nyakundi ina mengi zaidi

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Akizungumza mjiniGenevabwana Kay amesema kuwa usalama kwa sasa ndiyo changamoto kubwa inayolikabili taifa laSomaliana kuongeza kuwa kuwashinda kwa Al-shabab ndiyo njia ya kipekee ya kuleta amani na usalama katika taifa hillo.

Amesema kuwa tisho kutoka kwa makundi ya wanamgambo imevuka mipaka ya nchi hiyo akitoa mfano wa shambulizi la mwishono mwa wiki mjiniNairobinchiniKenya.

Bwana Kay amesema hata baada ya jangahilona baada ya mauaji yaliyofanywa na Al Shabaab, nchiniSomaliakwa sasa  kuna fursa nzuri ya kuisaidia nchi hiyo kuwa na amani na maendeleo. Hata hivyo, amesema kuna changamoto kadhaa ambazo zimesalia.

"Kwa sasa kuna serikali iliyotambuliwa kimataifa nchini Somalia. Kuna uungwaji mkubwa wa kimataifa na kikanda kwa taifa la Somalia na serikali inaedelea kudhibiti miji na maeneo mengi ya nchi. Lakini changamoto  zemesalia. Haki za binadamu ni moja ya chamagmoto kubwa zinazotukabili. Lakini hakuma hatua yoyote tunayofanya nchini Somalia iwe ya kisiasa inayoweza kufanikiwa ikiwa changamoyo za usalama hazitatatuliwa."

la mwishono mwa wiki mjini Nairobi nchini Kenya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930