Misri imo mbioni kuhitimisha kipindi cha mpito, Waziri Nabil Fahmy

Kusikiliza /

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil Fahmy, ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa  kipindi cha serikali ya mpito kitamalizika ifikapo mwisho wa msimu wa baridi hapo mwakani.

Katika hotuba yake mnamo siku ya Jumamosi, Bwana Fahmy pia amesema wananchi wa Misri walikuwa na kila sababu ya kuenda mitaani na kufanya maandamano, ili kutoa ujumbe kuwa wana uhuru na haki ya kuamua mustakabali wa nchi yao, na kwamba wapo tayari kukabiliana na wale wanaukiuka uhuru huo.

"Katika hili, watu wa Misri waliuonyesha ulimwengu kuwa, nia ya watu haiwezi kuvunjwa , na raia wana uwezo wa kuwapa viongozi mamlaka na pia kuwapokonya mamlaka hayo. Raia wa Misri wana ndoto kubwa kwa ajili ya siku zijazo, ambayo inaweza kufikiwa kupitia juhudi za utaratibu, katika muda unaokubalika."  

Waziri Nabil Fahmy amesema kuwa ndoto hiyo ya raia wa Misri inaenda sambamba na ndoto za watu kote duniani, kama ilivyo katika kanuni za kimataifa. Ameongeza kuwa serikali ya mpito ya Misri sasa hivi inaendelea kwenye mkondo wa kuweka mustakabali unaokubalika na wote.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031