Masoko ya ndani na ya kikanda yanaweza kuchangia ukuaji wa uchumi: UNCTAD

Kusikiliza /

Dr. Mukhisa Kituyi

Miaka mitano baada ya mdororo wa uchumi duniani kumalizika, bado uchumi wa dunia umesalia kuwa wenye msukosuko kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kupitia kwa ripoti ya kila mwaka kuhusu biashara na maendeleo UNCTAD inasema kuwa nchi zilizostawi ni lazima zichukue hatua za haraka kuabini chanzo cha hali hili mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia. Mkurugenzi mkuu wa UNCTAD daktari Mukhisa Kituyi anasema kuwa nchi zinazoendela ambazo zinatagemea mauzo ya bidhaa kwenye masoko ya kigeni kwa maendeleo zinastahili kubadili mikakati yao na kuangazia ziadi masoko ya ndani na yale yaliyo kwenye kanda zao.

(SAUTI YA MUKHISA KITUYI)

"Mdororo huko Marekani, kuendelea kudumaa kwa uchumi huko Ulaya ni kielelezo cha kutoweka kwa dhana iliyozoeleka ya ukuaji unaotegemea uuzaji bidhaa nje ya nchi. Na zaidi ya hilo la kuelekeza utegemezi kwa biashara ya nje, maendeleo sasa yanahitaji kuweka mizania ya kutosha kati ya soko la ndani na yale ya kikanda. Ujumbe muhimu wa kuendeleza uchumi unaoukua ni ushirikiano wa kikanda. Wakati zamani ushirikiano huo ulimaanisha uwekezaji moja kwa moja wa vitegauchumi, sasa hivi una maana nyingine kabisa ni kupanua wigo wa usafirishaji wa bidhaa na huduma kwenye ukanda husika ili kuziba pengo la utegemezi kwenye masoko ya nje ambayo sasa hayatabiriki."

UNCTAD inasema kuwa ukuaji wa uchumi hautarajiwi kuwa mkubwa mwaka huu na huenda ukadorora kwa asilimia 2.1 ikilingishwa na asilimia 2.2 ya mwaka uliopita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031