Malaysia yataka suluhu jumuishi la kisiasa kwa mzozo wa Syria

Kusikiliza /

Waziri Mkuu wa Malaysia

Malaysia imetoa wito kuwepo suluhu la kisiasa kupitia harakati zinazowajumuisha wote nchini Syria.

Akitoa hotuba yake wakati wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Waziri Kuu wa Malaysia, Mohd Najib Tun Abdul Razak, amesema taifa la Malaysia linapinga hatua yoyote isowajumuisha wote katika kuutatua mzozo wa Syria. Amesisitiza kuwa pande zote ni lazima zije pamoja na kutafuta suluhu la kisiasa.

Tunakaribisha makubaliano ya mkakati ulioongozwa na Marekani na Urusi, tunalaani vikali matumizi ya silaha za kemikali, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza juhudi za kutafuta njia za kidiplomasia za kuleta amani chini ya Umoja wa Mataifa. Ni lazima pia tutafute mtazamo na nia ya kisiasa ya kutafuta suluhu la haki kwa ajili ya Palestina. Tunatataraji kuwa hatua za kupatikana taifa huru la Palestina, kutokana na mipaka ya kabla ya mwaka 1967, na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu, zitafanywa.

Waziri huyo Mkuu wa Malaysia ameelezea matumaini yake kuwa Marekani na wanachama wengine wa nchi nne husika wataendelea kutoa mchango wao kama wapatanishi wa kuaminika katika harakati hizo. Amesisitiza kuwa ni kupitia katika amani tu ndipo kutakuwepo maendeleo na utu kwa watu wa Palestina.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930