Mafanikio makubwa yapatikana katika kukabiliana na Ukimwi

Kusikiliza /

Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu, Global Fund umetangaza hii leo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi pamoja na kinga kwa maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwamtoto. Matokeo yanaonyesha kuwa hadi Julai mwaka huu watu milioni mano nukta tatu wanaoishi na virusi hivyo wanapata dawa za kupunguza makali ya virusi chini ya mipango inayopata usaidizi wa mfuko huo wa kimataifa ikiwa ni ongezeko ikilinganishwa na wagonjwa Milioni Nne nukta Mbili mwishoni mwa mwaka jana. Halikadhalika kuna ongezeko la asilimia 21 la wajawazito wanaopata tiba kuzuia maambukizi ya virusi kwa watoto. Mkuu wa Global Fund Mark Dybul amesema taarifa hizo njema zinaonyesha kuwa jamii inaweza kudhibiti magonjwa hayo iwapo itafanya kazi kwa ushirikiano.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031