Maelfu ya watu wahama makwao kufuatia mapigano kaskazini mwa Kenya

Kusikiliza /

Maelfu ya watu bado wamehama makwao kwenye wilaya ya Moyale iliyo kaskazini mwa Kenya iliyo karibu na mpaka na Ethiopia kufuatia machafuko ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu kumi tangu kuanza kushuhudiwa tarehe 30 mwezi Agosti. Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa hayajafanikiwa kufanya tathmini kuhusu mahitaji ya kibinadamu yaliyo muhimu katika kutoa misaada kwa wale wanaotaabika.

Siku mbili za mapigano ya kikabila katiya makabila ya Gabra, Burji na Borana yamesabaisha kuchomwa kwa nyumba na kufungwakwa biashara kwenye maeneo ya Somare na Teti. Maafisa wanaohusika na elimu wanasema kuwa karibu shule 32 za msingi za zile za upili zimesalia zimefungwa wilayani Moyale tangu tarehe mbili mwezi huu baada ya wanafunzi na walimu kukimmbia makwao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930