Machafuko ya kidini Nigeria yahitaji suluhu

Kusikiliza /

Rais wa Nigeria Goodluck Ebele Jonathan

Machafuko ya kidini ya hivi karibuni nchini Nigeria na hususani katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ni moja ya ajenda kuu zilizotawala mkutano baina ya Rais Goodluck Ebele Jonathan na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.

Walipokutana kando ya mjadala wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wawili hao pia amezungumzia suala la kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia raia. Ban amemuhakikishia Rais Jonathan ushirikiano na msaada wa Umoja wa Mataifa katika juhudi za kurejesha amani na usalama , na kuwalinda raia Kaskazini mwa Nigeria.

Viongozi hao pia wamebadilishana mawazo kuhsu mafanikio yaliyopatikana nchini Mali, Guinea-Bissau na katika kutekeleza makubaliano ya Greentree baina ya Nigeria na Cameroon. Mwisho Ban amesisitiza umuhimu wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 na amekaribisha jukumu ambalo Nigeria italibeba kama mwenyekiti mwenza wa kamati ya kimataifa ya fedha na maendeleo endelevu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29