Leo ni siku ya kimataifa ya masuala ya shughuli za majini

Kusikiliza /

Leo ni siku ya kimataifa ya masuala ya shughulli za majini. Katika ujumbe wake maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku hii ambayo huadhimishwa Septemba 26 kila mwaka safari hii imeangukia katika wakati muhimu , wakati ambao Umoja wa Mataifa unaongoza katika juhudi za mwisho za kufikia malengo ya kimataifa ya kushughulikia madhila kupitia malengo ya maendeleo ya milenia, huku ikiweka mikakati na mtazamo wa ajenda za baada ya mwaka 2015.

Ban amesema juhudi zinazoendelea wanathmini usafiri wa majini kwani wa gharama nafuu na unahifadhi nishati katika mzunguko wa kimataifa. Ametoa wito wa kutumia fursa hii na siku hii kukumbusha wajibu na majukumu ya matumizi mazuri na udhibiti wa usafiri wa majini ili kusaidia kuunga mkono maendeleo endelevu.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930