Kuna wahamiaji wa kimataifa milioni 232 wanaoishi nje ya nchi zao:UM

Kusikiliza /

Kwa mujibu wa takwimu mpya za Umoja wa Mataifa zilizotolewa Jumatano kuna wahamajiaji wa kimataifa waliozaliwa kanda ya kusini wanaishi katika nchi zingine za Kusini kama ilivyo za Kaskazini.

Takwimu zinasema hii inaonyesha mabadiliko ya mfumo kwa wahamiaji wa Asia , lakini kimataifa bado Marekani ni sehemu inayopendwa saana miongoni mwa wahamiaji.

Umoja wa Mataifa unasema hivi sasa watu wengi zaidi wanaishi nje ya nchi zao kuliko wakati mwingine wowote. Mwaka 2013 watu milioni 232 au asilimia 3.2 ya watu wote duniani ni wahamiaji wa kimataifa ikilinganishwa na watu milioni 175 mwaka 2000 au milioni 154 mwaka 1990

Takwimu hizo zimetolewa kama maandalizi ya mjadala mkubwa wa viongozi kuhusu uhamiaji wa kimataifa na maendeleo unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 ya mwezi Oktoba 2013 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031