Kumiminika kwa wakimbizi Uganda, serikali yaimarisha ulinzi dhidi ya ugaidi

Kusikiliza /

Wakimbizi kambini ya Hoima, Uganda

Nchini Uganda, kuendelea kumiminika kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao sasa wanahifadhiwa kwenye kambi moja huko Hoima, kumeibua wasiwasi wa uwezekano wa waasi kujipenyeza na kutishia usalama wa wakazi wa eneo hilo.

Imeripotiwa kuwa polisi nchini Uganda tayari wameanza kuchukua hatua kuimarisha ulinzi kama anavyoripoti John Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchiniUganda.

(Ripoti ya Kibego)

Hussein Nsobya wa cheo cha ukaguzi kutoka kurugenzi ya kupambana na ugaidi amesema hafutilii mbali uwezekano wa magaidi kujipenyeza nchin humo, chini ya mwavuli wa wale wanaotoroka mapigano nchin Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC).

Anasema magadi wanaweza kulishambulia eneo la bonde la ufa la Ziwa Albert juu ya ugunduzi wa mafuta ambayo serikali inaamini yataisaidia kuinua uchumi wake. Bwana Nsobya amewataka wakazi na viongozi asusani katika maeneo ya mpakani na hapa mjini Hoima kupeana habari kuhusu wahamiaji.

(Sauti ya Hussein Nsobya)

Wiki jana, msemaji wa jeshi la serikali yaUgandaCol. Paddy Ankunda alitangaza kukamatwa kwa wapiganaji kadha waliokwepa kundi la FARDC nchin DRC na kuingia nchinUgandabila idhini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031